Saudi Arabia na Marekani ni sababu ya kupatikana amani na utulivu dunia

Saudi Arabia na Marekani ni sababu ya kupatikana amani na utulivu dunia

Hayo yamesemwa na Imam wa msikiti mtukufu wa Makka alipokuwa mjini New York ambapo amesema kuwa Marekani na Saudi Arabia ndio sababu ya kupatikana amani na utulivu duniani, suala ambalo limeleta mshangao mkubwa kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Imam wa msikiti mtukufu wa Makka ilipokuwa katika kongamano la Markaz ya fungaman la ulimwengu wa Kiislamu liliofanyika mjini New York amesema alipokuwa anaojiwa kwamba Saudi Arabia na Marekani ni nguzo mbili ambazo zinaathari kubwa duniani katika kuhakikisha kuwa dunia inaelekea upande wa amani na utulivu na ukamifu wa kibinadamu.
“Sheikh Abdurrahman Assudeis” alisema katika mahojiano na Televishen ya Al-ahbaria kuwa: tunawaomea taufiki Trump na mfalme wa Saudi Arabia wafikie malengo yao ya kuifikisha dunia katika ubinadamu na utulivu.
Maelezo ya Imam wa msikiti mtukufu wa Makka yameshika kipaumele katika mitandao ya kijamii ambapo watumiaji wa mitadao ya kijamii wameeleza kuwa mazungumzo ya Imam huyo ni aina fulani ya kuusafisha uso wa serikali ya Marekani ulimwenguni.
Mmoja katika watumiaji wa mitandao ya kijamii anaandika baada ya kuashiria filamu ya mauaji yaliofanywa na wamarekani nchini Iraq na kusema kuwa: hii ndio serikali ambayo Sudeis anasema, dunia itapata amani na utulivu kupia serikali hiyo, huku wengine wakiandika kuwa: maneno ya Imam wa msikiti wa Makka ni ishara ya usaliti wa mauaji ya damu za Waislamu yaliofanywa na serikali ya Marekani.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky