Saudi Arabia na washirka wake waache kuzuia vyakula kuingia Yemen

Saudi Arabia na washirka wake waache kuzuia vyakula kuingia Yemen

Mmoja miongoni mwa viongozi wa umoja wa mataifa ameitaka Saudi Arabia na washirika wake waliovamia Yemen waache kuzuia kuingia kwa vyakula na mafuta kupitia bandari mbalimbali za kibiashara nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: msimamizi wa misaada ya kibinadamu katika umoja wa Mataifa nchini Yemen amesisitiza kuwa, serikali iliojiuzulu ya Yemen pamoja na umoja wa kiarabu ukiongozwa na Saudi Arabia waache kuzuia kuingia kwa vyakula na mafuta katika Bandari za kibiashara za nchi hizo.
Aidha ameongeza kusema kuwa: kwa tumetoa angalizo kuwa wayemen milioni 10 wako katika hatari ya kupatwa na ukame mpaka ifikapo mwishoni mwa mwaka, ambapo endapo hatua za makusudi hazitachukuliwa za kukabiliana na hali hiyo, bila shaka janga hilo litawapata wananchi hao.
Alimalizia kwa kusema kuwa, kwa hakika pia tulishatoa ripoti ya kupungua kwa uwingizaji wa vyakula katika kipindi cha hivi karibuni katika Bandari mbalimbali ya Musharaf katika bahari nyekundu, ambapo utawala wa Saudi Arabia huzipekuwa meli zote zinazofika katika Bandnari hiyo, jambo linalopelekea kuzorotesha harakati za Bandari hiyo.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky