Saudi Arabia yakataza kuzuru pango la (Hiraa) na (Jabali Nuru)

Saudi Arabia yakataza kuzuru pango la (Hiraa) na (Jabali Nuru)

Serikali ya Saudi Arabia imewazuia Mahujaji wa mji mtuku wa Makka kwenda kuzuru Jabal-nur na Ghari-hira ziliopo katika mji huo sehemu ambazo ndio alipewa utume wa bwna wetu Muhammad (s.a.w.w)

Shirika la habari Ahlulabayt (a.s) ABNA: wizara ya masuala ya Hiaja na Umrah nchini Saudi Arabia imezuia mahujaji kwenda kuzuru na kutembelea sehemu aliokuwa ameshushiwa ufunoa bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w) katika mji mtukufu wa Makka.
Kwa mujibu wa ripoti hii, wizara ya masuala ya Hija na Umra nchini Saudi Arabia, imezitangazia Taasisi zote zinazo jishughulisha na kupeleka Mahujaji katika miji ya Makka na Madina, kwamba mahojaji watakaoingia katika mji mtukufu wa Makka hawataruhusiwa kuzuru sehemu ya Gharuhira na Jabalun-nur, hivyo taasisi hizo zinapaswa kufuta ratiba za kwenda katika sehemu hizo.
Wizara hiyo imetangaza hatua hiyo na kufafanua kuwa, maamuzi hayao yamechukuliwa kwaajili ya kulinda usalama na afya ya Mahujaji na kujiepusha na makosa yanayotokea katika maeneo hayo.
Aidha akibainisha kuwa, sehemu kuna miinuko mikubwa ambayo inaweza kupelekea kwa baadhi ya mahujaji  kupoteza fahamu na kuanguka kutokana na kukosa hewa safi.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky