Saudi Arabia yazuia mahujaji kupiga picha katika msikiti wa Makka na Madina

Saudi Arabia yazuia mahujaji kupiga picha katika msikiti wa Makka na Madina

Kuanzia sasa utawala wa Saudi Arabia watoa hukumu na sheria mpya yakuto ruhusiwa mahujaji kupiga picha wanapokuwa katika msikiti wa Makka na Madina

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: utawala wa Saudi Arabia umeweka kanuni mpya inayowazuia mahujaji wanaokwenda kuzuru maeneo matakatifu nchini humo kuto piga picha wanapokuwa katika msikiti wa Makka na Madina.
Aidha serikali hiyo imewataka wasimamizi wa misafara ya kupeleka mahujaji nchini humo, wasambaza kanuni mpaya kwa wale wanaotaka kwenda kuzuru maieneo hayo, huku ikisisitiza kuwa kutoifuata kanuni hiyo kutakuwa na adhabu kali kwa muhusika.
Miaka kadha iliopita mahujaji walikuwa na uhuru wa kupiga picha katika baadhi ya maeneo ya misikiti hiyo mitakatifu hata kuchukua video kulikuwa kuna ruhusa ama kuanzia sasa haitakuwatena ruhusa hiyo.
Wizara ya mambo ya dini nchini humo imetangaza kuwa kuto fuata sheria hiyo katika msikiti wa Makka na Madina kutapelekea kuchukuliwa kwa kamera ya mvunjaji wa kanuni hiyo na hata rejeshewa kamera yake.
Hivi karibuni yahudi mmoja kutoka utawala haramu wa Israel alisambaza picha kadhaa alizopiga akiwa katika msikiti wa tukufu wa Madina, jambo ambalo lilileta mshangao mkubwa kwa Waislamu ambapo walitoa mitamo yao mbali mbali katika mitandao ya kijamii.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky