Saudia yazidisha Mashambulizi Yemen

Saudia yazidisha Mashambulizi Yemen

Majeshi dhalimu ya Saudia arabia na washirika wake yameendelea kufanya mashambulizi makali dhidi ya wananchi madhulumu wa Yemen, mashambulizi hayo yamelenga hospitali na makazi ya watu.

Shirika  la habari la ABNA linaripoti kuwa: Majeshi dhalimu ya Saudia arabia na washirika wake yameendelea kufanya mashambulizi makali dhidi ya wananchi madhulumu wa Yemen, mashambulizi hayo yamelenga hospitali na makazi ya watu.

Wakati hayo yanaendelea wananchi wa Yemen wamerusha makombora na kushambulia kambi za majeshi ya Saudia arabia na kusababisha hasara kubwa ikiwemo vifo vya makumi ya wanajeshi.

Mauji ya kinyama yanafanywa na Saudia arabia ikishirikiana na Marekani na Israel, huku jumuia ya umoja wa mataifa ikifumba macho na kulisahau kabisa suala la jinai za kivita zinazojiri nchini Yemen.

Hayo yakijiri, Mkuu wa wapigaji wa Yemen Abudlmalik al- Huthi ameapa kutojisalimisha kwa majeshi yanayoungwa mkono na Saudi Arabia. Kwenye hotuba yake iliyopeperushwa kupitia televisheni al-Huthi amesisitiza kuwa wayemen hawataruhusu maadui watawale nchini kwao na watapambana nao kwa mpaka hatua ya mwisho. Aidha aliwataka raia wa Yemen kuunga mkono kampeni za Wahuthi nchini humo. "Nawaomba kila raia kushirikiana na kuwaeleza kuwa leo tuna jukumu la kukabili uchokozi unaoelekezwa katika mipaka na maeneo mengine. Kila mtu ana wajibu wa kuunga mkono ajenda ya kijeshi kwa sababu ina umuhimu, yenye maamuzi na ya msingi. Hakuna hatari isipokuwa kwa wasiojali na wadhaifu."

Marekani ambayo inatoa usaidizi wa vifaa na kuongoza vita  kwa majeshi ya muungano wa Saudi, wiki iliyopita walishauri mapigano hayo yasitishwe lakini hilo halijatimia. Msemaji wa serikali Robert Palladino amesema Marekani imerejelea kauli yake kwa pande husika kuwa hakuna ushindi wa kijeshi utakaopatikana nchini Yemen.

Maelfu ya watu wasio na hatia wameuawa nchini Yemen, huku Marekani na Ufaransa na Uingereza zikinufaika kwa kuuza silaha kwa waarabu.

Mwisho wa habari / 291


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky