Sehemu ya mwisho ya kikundi cha Daesh katika mji wa Musol wakombolewa

  • Habari NO : 841003
  • Rejea : ABNA
Brief

Majeshi ya serikali ya Iraq yamefanikiwa kuikomboa sehemu ya mwisho ya kikundi cha kigaidi cha Daesh katika mji wa Musol wa zamani

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: majeshi ya serikali ya Iraq yametangaza kuwa sehemu ya mwisho ambayo kikundi ch kigaidi cha Daesh kilibaki sehemu wamefanikiwa kuikomboa kutoka mikononi mwa kikundi hicho.
Hayo yamesemwa na mkuu wa jeshi la polisi nchin humo amebainisha kuwa: majeshi ya nchi hiyo yamefanya mashambulizi yake ya anga wakishirikiana na masnaipa katika sehemu ya mwisho iliobaki kikundi cha kigaidi cha Daesh na kufanikiwa kuimiliki sehemu hiyo, huku wakigundua maghala ya makombora mbalimbali ya kikundi hicho cha kigaidi.
Aidha majeshi hayo pia yamefanikiwa kuona sehemu ya mafunzo ya kikundi hicho iliokuwa chini ya ardhi kwa urefu wa mita kumi, ambapo sehemu hiyo ya mafunzo waliipa jina la kambi ya Abu masudi ambayo ilikuwa maeneo yanayoitwa Albusaef maghiribi mwa Musol nchini Iraq.


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Arba'een
Mourining of Imam Hossein
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky