Serikai ya Uingereza yatangaza kuweko magaidi 350 nchini humo

Serikai ya Uingereza yatangaza kuweko magaidi 350 nchini humo

Majeshi ya ulinzi na usalama ya Uingereza watangaza kuweko zaidi ya magaidi 350 nchini humo, ambao kwa muda kadhaa walikuwepo nchini Syria na Iraq ambapo walikuwa pamoja na kikundi cha kigaidi cha Daesh, huku wakisistiza kuwa magaidi hao muda wowote wanaweza kufanya tukio lakigaidi nchi humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kwa mujibu wa habari hii ni kwamba vyombo vya ulinzi na usalama vya Uingereza vimtambua uwepo wa magaidi kwa uchache 350 ambao muda mrefu walikuwa pamoja na kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini Iraq na Syria, ambapo fani za kufanya matukio ya kigaidi wanazifahamu.
Wahariri wa mambo ya usalama wakiashiria kuwepo kwa idadi hiyo, wamesema kuwa: magaidi hao walio na utaifa wa nchi hiyo, kwakuwa wamepata mafunzo kamili ya kigaidi, ni tisho kubwa kwa amani ya taifa.
Gazeti la Tems la Uingereza pia limeashiria idadi hiyo na kusisitiza ongezeko la idadi hiyo inatishia amani ya nchi hiyo kutokana na kuwepo magaidi ambao ni wananchi wa taifa hilo.
Inasemekana kwamba tukio la mwisho la kigaidi liliotokea nchini humo, lilitokea tarehe 22 mwezi machi mwaka huu katika moja ya midani za mji mkuu wa nchi hiyo, ambapo tukio hilo limesababisha vifo vya wananchi watano na kujeruhiwa kwa watu zaidi ya 40 nchini humo.
Kwa mujibu wa takuwimu iliotangazwa nchini humo ni kwamba mpaka sasa watu zaidi ya 800 ambao ni wananchi wa nchi hiyo wamejiunga na kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini Syria na Iraq ambapo hivi sasa wapo pamoja na vikundi hivyo.
mwiaho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky