Serikali ya Iran yapinga madai ya Marekani kuhusu ugaidi

Serikali ya Iran yapinga madai ya Marekani kuhusu ugaidi

Serikali ya Jamhuri ya kiislam ya Iran leo hii imepinga vikali madai yaliyotolewa na waziri wa ulinzi wa Marekani James Mattis kwamba Iran ilikuwa ni msambazaji wa kwanza wa ugaidi na kusema chanzo kikuu cha ugaidi ilikuwa ni Saudi Arabia ambao ni washirika wa karibu wa Marekani, ambapo Marekani na Saudia arabia wanashirikiana kutuma magaidi nchini Syria, Iraq na Yemen ili kufanikisha malengo yao ya kisiasa.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Serikali ya Jamhuri ya kiislam ya Iran leo hii imepinga vikali madai yaliyotolewa na waziri wa ulinzi wa Marekani James Mattis kwamba Iran ilikuwa ni msambazaji wa kwanza wa ugaidi na kusema chanzo kikuu cha ugaidi ilikuwa ni Saudi Arabia ambao ni washirika wa karibu wa Marekani, ambapo Marekani na Saudia arabia wanashirikiana kutuma magaidi nchini Syria, Iraq na Yemen ili kufanikisha malengo yao ya kisiasa.

Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni Bahram Ghasemi amenukuliwa alipokuwa akizungumza na chombo cha habari cha serikali cha Iran IRNA akisema baadhi ya nchi zilizoongozwa na Marekani zimeamua kupuuzia chanzo kikuu cha ugaidi wa makundi ya Takfiri Wahhabi na itikadi kali. Alikuwa akiangazia makundi ya Waislamu wa madhehebu ya Sunni na fikra za kiislamu za itikadi kali za Wahhabi zenye makao makuu yake Saudi Arabia.

Ghasemi alikuwa akijibu matamshi yaliyotolewa na Mattis hapo jana baada ya kutakiwa kutoa maoni yake kuhusu maoni aliyoyatoa mwaka 2012 kwamba vitisho vitatu vikuu ambavyo Marekani ilikuwa inakabiliana navyo vilikuwa ni Iran pekee.

Ikumbukwe kuwa Iran ndio nchi ya kwanza kutuma majeshi yake kwenda Iraq na Syria kuzisaidia nchi hizo kupambana na magaidi wa Daesh ambao wamekuwa wakipewa mafunzo na majeshi ya Marekani na kupata msaada ya kifedha na kijeshi kutoka Saudia arabia, Qatar, Uturuni na Jordan.

Na mpaka sasa majeshi ya Iran bado yanaendelea kupambana na ugaidi katika ardhi za Syria na Iraq.

Mwisho wa habari/ 291

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky