Serikali ya Iran yatoa onyo kwa Saudia arabia na washirika wake

Serikali ya Iran yatoa onyo kwa Saudia arabia na washirika wake

Ndege za majeshi ya muungano unaoongozwa na Saudi Arabia zimeshambulia makazi ya wananchi ya mji mkuu alfajiri ya leo baada ya wapiganaji wa Huthi kumuua rais wa zamani Ali Abdullah Saleh ambaye alikuwa ni mamluki wa Saudia arabia wakati akikimbia kutoka mji huo kufuatia kuvunjika kwa muungano wao wakazi wa mji huo wamesema.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Rais wa Jamhuri ya kislamu ya Iran Hassan Rouhani amesema : Wayemeni watawafanya wale wanaoishambulia nchi yao wajutie vitendo vyao,  wakati  muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia ukishambulia mji mkuu wa Yemen na kuuwa raia hovyo.

Mtoto wa rais wa  zamani  wa  Yemen Ali Abdallah  Saleh , aliyeuwawa na wanamgambo  wa  kihuthi , alitoa wito  wa  kulipiza  kisasi  dhidi wapiganaji wa Huthi. "Watu  wa  Yemen  wanawafanya  wachokozi wajutie hatua walizochukua," Rouhani  amesema hayo  katika  hotuba  iliyotangazwa moa  kwa  moja  katika  televisheni. Matamshi  yake  yanakuja  siku moja  baada  ya  kuuwawa  rais  wa  zamani  Ali  Abdallah Saleh na wapiganaji wa Huthi  baada ya kuwasaliti wapiganaji hao. mashambulizi  makali  kutoka  kwa  majeshi kutoka nchi 11  yanayoungwa  mkono  na Saudi  Arabia  dhidi  ya wananchi wa mji  mkuu  wa  Yemen Sanaa.

Kamanda  wa ngazi ya juu wa Jeshi la Iran, Mohammad Ali Jafari , amesema  Saleh aliuwawa  kwasababu  alikuwa  akijaribu kufanya mapinduzi ya kuuondoa  uongozi  wa  Wahuthi  kutoka  madarakani.

Saleh  hivi  karibuni  alivunja ushirikiano  wake na wapiganaji wa Huthi  ambao wanatetea wananchi, uliodumu  kwa  muda  wa  miaka  mitatu  na  kusema yuko tayari kwa  kufanya sulhu na kuungana na Saudia arabia ambayo imeua na kujeruhi mamilioni ya wananchi wa Yemen.

"Wasaliti  Saudi Arabia  wanataka  kuleta  hali  ya  wasi  wasi  wa kiusalama  katika  eneo hili chini  ya  amri  kutoka  Marekani wakifanyakazi  kwa  pamoja  na  Israel , tumeshuhudia juhudi  zao  za kuanzisha  mapinduzi  dhidi  ya  Wahuthi, ambayo yamekabwa mapema kabla  ya  kuzaliwa.

Ndege  za  majeshi  ya  muungano  unaoongozwa  na  Saudi Arabia zimeshambulia  makazi ya wananchi ya  mji  mkuu  alfajiri ya  leo  baada  ya  wapiganaji wa Huthi  kumuua  rais  wa  zamani  Ali Abdullah Saleh  ambaye alikuwa ni mamluki wa Saudia arabia wakati  akikimbia  kutoka   mji  huo  kufuatia kuvunjika  kwa  muungano  wao wakazi  wa  mji  huo  wamesema.

Wito wa kupambana  na  Wahuthi

Rais  ambaye wananchi hawamgitaji ambaye amekimbilia Sadia Abedrabbo Mansour Hadi  ametoa wito kwa  Wayemeni  kujiunga  pamoja  dhidi  ya  wapiganaji wa Huthi. Karibu  mashambulio  saba yameangukia  katika  jengo  la makao  makuu  ya  rais  katika  eneo linaloishi  watu  wengi   katikati  ya  mji  wa  Sanaa, na kusababisha maafa makubwa, wamesema watu  walioshuhudia.

Kumekuwa  na mapambano  madogo  madogo  kati  ya  Wahuthi  na waungaji  mkono  wa  Saleh  katika  wilaya  za  kusini  ambazo zimekuwa  ni  ngome  kuu  ya  waungaji  wake  mkono.

Nae  mtoto  wa  rais  wa  zamani  Ali Abdullah Saleh  aliyeuwawa ametoa  wito  wa  kulipiza  kisasa dhidi  ya  wapiganaji wa Huthi.

"Nitaongoza  mapambano  hadi  Mhuthi  wa  mwisho atakapoondo9lewa  kutoka  Yemen, damu  ya  baba  yangu itasikika katika  masikio  ya  Iran, "  alinukuliwa  Ahmed Ali Saleh  akisema. Amewataka  waungaji  mkono wa  baba  yake , "kuirejesha  Yemen kutoka  mikono  ya  wanamgambo  wa  Kihuthi wanaopambana na maadui wa Yemen".

Mkuu wa Umoja  wa  nchi  ya  Kiarabu  Arab League  Ahmed  Abdul Gheit ameshutumu  leo  kuuwawa  kwa  rais  wa  zamani  wa  Yemen na  wapiganaji wa  Kihuthi, akisema  hali  hiyo  inaelezea  juu  ya  hali msingi  wa uhalifu wa  kundi  hilo. Mkuu  huyo  wa  jumuiya  ya mataifa  ya  Kiarabu  ameonya  kwamba  kuuwawa  kwa  Saleh  siku ya  Jumatatu  kunatishia  kuripuka kwa  hali  mbaya ya  usalama , katika  nchi  hiyo  iliyoharibiwa  kwa  vita.

Mwisho wa habari / 291

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Arba'een
Mourining of Imam Hossein
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky