Serikali ya Iraq yaamua kuwarejesha watu 300 kutoka familia za Daesh mataifani mwao

Serikali ya Iraq yaamua kuwarejesha watu 300 kutoka familia za Daesh mataifani mwao

Serikali ya Iraq imeamua kuwarejesha katika mataifa yao watoto na wanawake 300 wa kikundi cha kigaidi cha Daesh waliokuja kutoka mataifa mengine walikuwa pamoja na magaidi hao

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA:  serikali ya Iraq imetangaza rasmi lengo lake la kuwarejesha katika mataifa yao wanawake na watoto 300 ambao waume na baba zao walikuwa katika kikundi cha kigaidi cha Daesh, ambao walibaki katiuka mji wa Musol baada ya mji huo kuingia mikononi mwa serikali ya Iraq na kusambaratishwa kwa magaidi hao.
“Nuru Dini Kabalani” ambaye ni naibu spika wa bunge la Iraq amebainisha kuwa mpango huu ni hatua ya pili ambayo ni yakuwarejesha katika mataifa yao wa familia za magaid hao wa Daesh na hatua zingine zifuatazo watarudishwa watu 1200 wakiwa ni familia ya magaidi hao.
Familia za magaidi baada ya kusambaratishwa kwa magaid hao katika mji wa Musol, serikali ya Iraq ilizichukua familia hizo na kuzihamishia ya (Talkif) kaskazini mwa Musol, ambapo watu wote waliokamatwa ni wanawake 509 na watoto 813 ambao wanautaifa wa natifa 13 kutoka bara la Ulaya Asia.
Miongoni mwa wanake hao 509 wa kikundi cha kigaidi cha Daesh 300 kati yao wanatokea nchini Uturuki, huku kwa upande mwingine mataifa husika yako tumbo joto kutokana na kurudi kwa familia hizo za kigaidi katika maifa hayo, ikiwemo mataifa ya Ulay kwakile wanachokidai kuwa watu hao wanatishia amani ya mataifa hayo watakaporudi ndani ya mataifa hao.  
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky