Serikali ya Qatar iko tayari kwa majadiliano kumaliza mgogoro wa Ghuba

Serikali ya Qatar iko tayari kwa majadiliano kumaliza mgogoro wa Ghuba

Saudi arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu zikuiungwa mkono na Misri na serikali ya Yemen ya zamani, zilitangaza kuvunja uhusiano wa kibalozi na Qatar, kwa madai kwamba nchi hiyo inafadhili ugaidi nchini Syria na Yemen na ina uhusiano wa karibu na Iran, ambapo Qatar ilipinga kuwa Iran si tishio wala adui wa nchi za kiarabu na kuyashauri mataifa ya kiarabu kuchunguza adui yao halisi.

Shirika la habari la ABNA linaripot kuwa: Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Qatar amekiambia kituo cha matangazo cha Al Jazeera kinachofadhiliwa na taifa hilo, kwamba nchi yake na Marekani zinaendelea kuwasiliana na Mfalme wa Kuwait, ambaye anaongoza juhudi za upatanishi katika mgogoro wa kidiplomasia wa wiki moja sasa katika Ghuba.Sheikh Mohammed bin Abdulrahman al-Thani alisema wako tayari kuyajadili mapendekezo yoyote yatakayotolewa, lakini hadi sasa hawakupata jibu kuhusu hilo. Alisema mazungumzo ya kibalozi ndiyo suluhisho lakini hilo linahitaji msingi ambao bado haujapatikana. Saudi arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu zikuiungwa mkono na Misri na serikali ya Yemen ya zamani, zilitangaza kuvunja uhusiano wa kibalozi na Qatar, kwa madai kwamba nchi hiyo inafadhili ugaidi nchini Syria na Yemen na ina uhusiano wa karibu na Iran, ambapo Qatar ilipinga kuwa Iran si tishio wala adui wa nchi za kiarabu na kuyashauri mataifa ya kiarabu kuchunguza adui yao halisi.

Mwisho wa habari / 291

 

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky