Serikali ya Uturuki yajenga ukuta katika sehemu wanayopakana na Iran+ picha

Serikali ya Uturuki yajenga ukuta katika sehemu wanayopakana na Iran+ picha

Serikali ya Uturuki imekususdia kujenga ukuta kwaajili ya kuzuia kuingia magaidi na wahalifu nchini humo ambapo ukuta huo unajengwa katika sehemu inayopakana nchi hiyo na Iran

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: serikali ya Uturuki imeanza rasmi kutengeza ukuta wa ulinzi katika mpaka wa Iran.

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya Uturuki ni kwamba ukuta huo unafanan na ukuta wa kilometa 910 ambao Uturuki umeujenga katika mpaka wa nchi hiyo na Syria

“Sulaiman Alban” mkuu wa mkoa wa Aghure ulipo mashariki mwa Uturuki amekwenda kufanya ukaguzi maendeleo ya utekelezaji wa mpango huo, huku akisadikiwa kuwa asilimia kubwa ya wanaokaa katika mkoa huo ni waturuki wa kabila la Adhariy na wakurdi.

Kwa mujibu wa yale yalioelezwa katika vyombo vya habari vya Uturuki ni kwamba: ukuta huo utajengwa kwa kutumia zege na utakuwa na urefu wa mita tatu.

Lengo la serikali ya Uturuki katika kujenga ukuta huo ni kuzuia wahalifu kuingia nchini humo, kadhalika kuingiza mali kwa kukwepa kodi.

Rais wa Uturuki alitoa kauli ya kutengeza ukuta katika mipaka ya Iraq na Iran toka mwanzoni mwa mwaka huu wa 2017 kwa lengo la ulinzi na usalam.

Mkoa wa Azarbaijan ya Magharibi iliopo nchini imepakana na mikoa mine ya Uturuki eneo hilo linaukubwa wa kilometa 500 baina ya nchi hizo mbili.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky