Shambulio la kigaidi dhidi ya wafanya ziara ya Imamu Husein lagunduliwa kabla ya kufanikiwa

Shambulio la kigaidi dhidi ya wafanya ziara ya Imamu Husein lagunduliwa kabla ya kufanikiwa

Majeshi ya Usalama nchini Iraq kikosi namba 22 cha miguu kufuatia uchunguzi wake, kimefanikiwa kugundua shambulio la kigaidi liliokuwa limepangwa kufanywa siku maalumu dhidi ya wanaokwenda kufanya ziara ya arubaini ya Imamu Husein katika mji wa Karbala nchini Iraq

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: hayo yamesemwa na kamanda mkuu wa uchunguzi na mashambulio dhidi ya kikundi cha kigaidi cha Daesh mjini Baghdadi ametangaza kuwa majeshi ya ulinzi na usalama nchini Iraq wamefanikiwa kugundua mpango wa kikundi cha kigaidi cha Daesh cha kutaka kuwashambulia waliokwenda kufanya Ziara ya arubaini Imamu Husein nchini humo kabla ya kutekelezwa mpango huo.
Aidha majeshi ya Iraq wamefanikiwa kufikia tija hiyo baada ya kufanya uchunguzi na utafiti wa kina kunako sehemu waliokuwa wameandaa kufanyia shambulio hilo na kufanikiwa kuwasambaratisha magaidi hao na mpango huo.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky