Shambulio liliopangwa dhidi ya wanaokwenda ziara ya Arbaini ya Husein lateguliwa

Shambulio liliopangwa dhidi ya wanaokwenda ziara ya Arbaini ya Husein lateguliwa

Majeshi ya ulinzi na usalama ya Iraq leo yametangaza kusambaratisha na kutegua bomu liliokuwa limetegwa kwa lengo la kulipuliwa misafara wanaokwenda katika ziara ya Arubaini ya Imamu Husein, ambapo lilitegwa katika daraja la Assuwayrah kaskazini mwa mkoa wa Wasit nchini Iraq

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: tume ya ulinzi na usalama katika mji wa Suwayrah uliopo katika mkoa wa Wasit imetangaza kulisambaratisha bomu ambalo magaidi walipanga kufanya kitendo cha kigaidi dhidi ya wanaokwenda kufanya ziara ya Arubaini ya Imamu Husein katika mji wa Karbala ambao hupita katika sehemu hiyo.
Mkuu wa kamati hiyo ametoa kauli yakuwa: majeshi ya usalama ya sehemu hiyo leo yamefanikiwa kusambaratisha mpango wa magaidi wa Daesh wa kuwashambulio wanaokwenda kumzuru Imamu Husein siku ya arubaini, ambapo walitega bomu katika daraja moja la Suwayrah kaskazini mwa mkoa huo.
Bomu hilo limegunduliwa jeshi la Polisi la sehemu hiyo ambapo bomu hilo liliteguliwa kabla ya kuripuka kwake na kuleta hasara kwa wananchi na mali zao.
Inasemekana kuwa mkoa ya kusini mwa Iraq ikiwemo mkoa wa Wasit imebuni mpango maalumu wa kulinda usalama wa watu wanaokwenda ziara ya Arubaini ya Imamu Husein kwa miguu, ili waweze kuwalinda watu hao kutokana na mashambulio ambayo kikundi cha kigaidi cha Daesh kinaweza kikawashambulia wananchi hao, katika mpango huo wamelazimika kufunga baadhi ya barabara katika sehemu hizo.   
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Arba'een
Mourining of Imam Hossein
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky