Sheikh wa Azhar: kuwauwa magaidi ni wajibu wa kisheria

Sheikh wa Azhar: kuwauwa magaidi ni wajibu wa kisheria

Sheikh wa chuo cha Azhar Sharif nchini Misri amesema kwamba suala la jeshi la polisi na majeshi mingine kuuwa magaidi nchini humo ni suala la wajibu wa kisheria

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Sheikh Abbasi Shumani kaimu wa kiongozi wa sheikh wa Azhar ameyasema hayo alipokuwa anafanya mazungumzo na televishen ya Annahar, akisisitiza kuwa kuwauwa magaidi ni wajibu wa kisheria.
Aidha amebainisha kwa kusema kuwa: Sheikh mkuu wa Azhar (Ahmad Atwayib) anaameni kuwa jeshi la Polisi na majeshi mingine nchini humo, jambo lao kuwauwa magaidi ni jambo la wajibu wa kisheria, huku akifafanua kuwa fatuwa hiyo imepitishwa na masheikh wote wa chuo cha Azhar.
Hivyo basi sisi tunaamini kuwa magaidi hawana dini, bali huitumia dini kwaajili ya kuwakinaisha vijana kuhusu fikira zao potovu hatimaye kufanya mambo yasiofaa kwa kutumia mwamvuli wa dini.
mweisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky