Syria yakataa waangalizi wa Umoja wa mataifa kwenye maeneo salama

Syria yakataa waangalizi wa Umoja wa mataifa kwenye maeneo salama

Waziri wa mambo ya nje wa Syria Walid Muallem amesema nchi yake imekatalia mbali wasimamizi wa Umoja wa mataifa au vikosi vya kimataifa kusimamia maeneo manne ya yaliyotengwa kwa usalama wa raia, Umoja wa mataifa umekuwa ukitumiwa na Marekani kuwatorosha magaidi maeneo waliyozingirwa na majeshi ya Syria.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Waziri wa mambo ya nje wa Syria Walid Muallem amesema nchi yake imekatalia mbali wasimamizi wa Umoja wa mataifa au vikosi vya kimataifa kusimamia maeneo manne ya yaliyotengwa kwa usalama wa raia, Umoja wa mataifa umekuwa ukitumiwa na Marekani kuwatorosha magaidi maeneo waliyozingirwa na majeshi ya Syria.

Waziri huyo wa mambo ya nje wa Syria amesema Syria haitakubali mabadiliko yoyote mbali na yale yaliyokubaliwa na kutiwa saini na Urusi, Iran na Uturuki katika mji wa Astana nchini Kazakhstan.  Makubaliano hayo yalikuwa ni juu ya kutenga maeneo manne ya usalama ambapo pande zote zitasitisha mashambulio katika maeneo hayo pia sehemu hizo zitagawanywa kwa kuwekwa mipaka ya kiusalama yenye sehemu za kukagua watu kabla hawajavuka maeneo hayo ambapo wanajeshi wadhamini watasimamia kutokana na makubaliano hayo.

Makubaliano hayo yalianza kufanya kazi mnamo siku ya Jumamosi na yameleta hali ya utulivu.  Waziri wa mambo ya nje wa Syria amesema majeshi ya nchi yake yatajibu mashambulio yoyote au pindi makubaliano hayo yatakapovunjwa. Moallem amesema makubaliano hayo yatawezesha kusitishwa mapigano kufikishwa kwa haraka misaada ya kiutu na kuwapa wakimbizi wa ndani nafasi ya kuyafikia maeneo salama ambayo yametengwa katika mikoa minane ya nchini Syria.

Ijapokuwa serikali ya Syria na makundi ya magaidi wanaodhaminiwa na Marekani hawakutia saini moja moja makubaliano hayo yaliyofikiwa katika mji wa Astana, waziri wa mambio ya nje wa Syria Walid Muallem amesema leo serikali ya Syria imepitisha maamuzi hayo.

Al Muallem amesema serikali yake imetafuta njia mbadala baada ya mazungumzo ya kutafuta amani kushindikana kwa hivyo serikali yake imekuwa inatekeleza makubaliano na maridhiano ya ndani ya nchi. 

Makubaliano hayo hayazingatii maeneo ambako kwa sasa vita dhidi ya wapiganaji wa kundi  la kigaidi la Daesh linalojiita Dola la Kiislamu IS vinaendelea katikati ya Syria na katika maeneo ya Mashariki na Kaskazini.  Wapiganaji wa Daesh wanakabiliwa na mashambulio makali kutoka kwa vikosi vya serikali ya Syria.

Waziri huyo wa mambo ya nje wa Syria Walid Muallem amesema mapambano yanayoendelezwa na kikosi cha SDF dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh ni sawa kabisa na serikali yake inatambua na kuunga mkono vita hiyo. Pili Muallem amesema iwapo raia wa Kikurdi walio nchini Syria wanashiriki katika mapambano dhidi ya makundi ya kigaidi vilevile ni hatua ambayo inakubalika kisheria kwa sababu Wakurdi hao wanapambana na makundi ya kigaidi ndani ya ardhi ya Syria. Watu zaidi ya 320,000 wameuwawa nchini Syria tangu mgogoro unaochochewa na Marekani na washirika wake kuzuka nchini humo mnamo mwaka 2011.

Mwisho wa habari/ 291

 

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky