Tetemeko la ardhi latokea magaharibi mwa Iran; 445 wapoteza maisha na 7100 wajeruhiwa

Tetemeko la ardhi latokea magaharibi mwa Iran; 445 wapoteza maisha na 7100 wajeruhiwa

Tetemeko la ardhi liliokuwa na kiwango 7.3 latokea katika miji ya magharibi mwa Iran na kusababisha hasara kuwa ya mali na vifo vya wananchi ambapo mpaka sasa watu 445 wamepoteza maisha huku ikisadikiwa kuwa watu 7100 wamejeruhiwa huku ikielezwa kuwa kunauwezakano mkubwa wa kuongezeka kwa vifo viliotangazwa.

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: tetemeko kubwa la ardhi limetokea ambalo lilikuwa na kiwango cha 7.3 katika mkoa wa Kermanshah, ambapo baada ya muda mchache lilitokea katika mipaka ya Iraq na Iran, tetemeko hilo la ardhi limehesiwa kutokea katika mikoa mingi ya magharibi mwa Iran nakuleta madhara makubwa katika sehemu hizo.
Mikoa iliopata tetemeko hilo ni Hmadani, Araki, Zanjan, Ahwazi, Iilam, Sanandaj, Kermanshah, Tabriz, Urumiyeh, Ardabil na mikoa mingine pia ilihisi tetemeko hilo.
Aidha baadhi ya habari zinaeleza kuwa mikoa mingine kama Markaziy, Azarbaijann Shargiy, Azarbaijan Gharbiy, Kurdistan, Kguzestani na Bushehri ilikubwa na tetemeko hilo.
Ama habari zinaashiria kuwa mkoa uliokuwa umeathirika zaidi ni mkoa wa Kirmanshah, ambapo maeneo mengi ya mkoa huo zimeharibika ikiwemo miundombinu yake kama maji, umeme na Gesi, huku wizara ya afya ikitangaza kuwa mpaka sasa watu 445 wamepoteza maisha na wengine 7100 kujeruhiwa kufuatia tetemeko.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky