Trump: aomba kukabiliana na Iran

Trump: aomba kukabiliana na Iran

Rais wa Marekani katika mazungumzo yake na mfalme wa Oman, amemtaka mfalme huyo kukabiliana na serikali ya Iran

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: “Donald Trump” Rais wa Marekani amezungumza kwa simu na mfalme Qabus wa Oman.
Kwa mujibu wa kauli ya ikulu ya Marekani kuhusu mazungumzo hayo imeeleza kuwa: Rais wa Marekani amesisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano kati ya pande hizo mbili, huku wakizungumzia suala la utatuzi wa matatizo yaliopo katika ukanda wa mashariki ya kati.
Aidha katika kauli ya ikulu ya Marekani imeongeza kusema kwamba: “Rais wa Marekani Donald Trump amesisitiza suala la kukabiliana na harakati za jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika ukanda wa mashariki ya kati.
Ombi la Trump la kukabiliana na serikali ya Iran limetokea katika hali ambayo wiki moja kupita baada ya waziri wa mambo ya nje wa Oman kufanya safari isiokuwa imepangwa kabla kwenda nchini Iran na kufanya vikao mbalimbali na viongozi wa serikali ya jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Kwa mujibu wa maelezo ya viongozi wa Iran na Marekani ni kwamba serikali ya Oman ndio muunganishaji wa nchi hizo mbili katika kuanza kufanya mazungumzo ya mpango wa nyuklia wa Iran.
Vyombo vya habari vya marekani siku kadhaa ziliopita vilitangaza kuwa serikali mpya ya Marekani inafanya juhudi kubwa ya kuishinikiza Oman, kujitenga na kuwa mbali na serikali ya jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

mwisho/ 290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky