Trump na Putin wakubaliana kumaliza mgogoro wa Syria

Trump na Putin wakubaliana kumaliza mgogoro wa Syria

Rais wa Marekani Donald Trump ambaye anaunga mkono upande wa wapinzani na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin ambaye anaunga mkono serikali wamekubaliana kuwa mzozo wa Syria hauwezi kumalizwa kwa nguvu za kijeshi bali kisiasa.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Rais wa Marekani Donald Trump ambaye anaunga mkono upande wa wapinzani na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin ambaye anaunga mkono serikali  wamekubaliana kuwa mzozo wa Syria hauwezi kumalizwa kwa nguvu za kijeshi bali kisiasa.

Viongozi hao walitoa tamko la pamoja pembezoni mwa Mkutano mkuu wa viongozi wa jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi wa nchi za Asia na Pacifiki (APEC) katika mji wa Da nang nchini Vietnam. Trump na Putin pia wameeleza kwamba watashirikiana katika juhudi za kupambana na kundi la kigaidi la Daesh linalojiita Dola la Kiislamu IS.

Walizungumza baada kuwepo tashwishi hapo awali kama viongozi hao wangelikutana. Taarifa kutoka Ikulu ya Rais wa Urusi zimesema tamko la marais hao limeonyesha kuridhika kwa viongozi hao kutokana na juhudi za kuzuia mivutano baina ya majeshi yao yaliyoko nchini Syria.

Jeshi la Urusi hivi karibuni limekuwa likiilaumu Marekani kwa kujifanya inapambana na kundi la kigaidi la Daesh  nchini Iraq na pia kwa kuizuia operesheni dhidi ya magaidi hao inayoungwa mkono na Urusi mashariki mwa Syria.

Trump na Putin wazungumzia uchaguzi wa Marekani 2016 

Kwa upande mwingine, Trump amesema Rais wa Urusi Vladimir Putin amemwambia kuwa hakuingilia uchaguzi wa Marekani wa mwaka ambao matokeo yake yalipelekea yeye kuingia madarakani.

Kiongozi huyo wa Marekani amewaambia wanahabari kuwa kila mara Putin anapokutana naye humueleza kuwa hakuingilia uchaguzi wa Marekani na anaamini kile anachomwambia kuwa ukweli.

Uhusiano wa Trump na Urusi umekuwa gumzo katika mwaka wake wa kwanza tangu aingie madarakani huku baadhi ya wasaidizi wake wakifanyiwa uchunguzi kwa madai ya kushirikiana na Urusi.

Rais wa Urusi amemtaja Trump kuwa mtu mwenye heshima na rahisi kutangamana naye akiongeza kuwa hawafahamiani sana lakini amepata taswira kuwa Rais Trump ni mtu muungwana na mcheshi.

Alipoulizwa na wanahabari kuhusu madai nchi yake iliingilia uchaguzi wa Marekani, Putin amesema hizo ni ndoto tu zilizo na lengo la kuhujumu utawala wa Trump.

Baada ya kutilia msisitizo mwaka jana wakati wa kampeini za uchaguzi wa Rais, Trump alisema litakuwa jambo jema iwapo Urusi na Marekani ziatshirikiana kuyatatua matatizo ya ulimwengu, viongozi hao wawili hawajaonekana kukutana mara kwa mara tangu Trump kuingia madarakani.

Trump Jumamosi ameuzuru mji mku wa Vietnam, Hanoi, kituo chae cha kumi katika ziara ya siku 11 barani Asia. Baada ya hapo anatarajiwa kuizuru Ufilipino Jumapili ambako atakutana na mwenyeji wake Rais Rodrigo Duterte.

Mwisho wa habari / 291


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky