Trump: Ujenzi wa makazi ya waisrael Palestina haufai kwa amani

Trump: Ujenzi wa makazi ya waisrael Palestina haufai kwa amani

Rais wa Marekani Donald Trump amesema haamini kuwa kuendelea kwa ujenzi wa makazi ya walowezi wa kiisrael katika ardhi ya Wapalestina

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Rais wa Marekani Donald Trump amesema haamini kuwa kuendelea kwa ujenzi wa makazi ya walowezi wa kiisrael katika ardhi ya Wapalestina ni hatua nzuri katika amani ya mashariki ya kati yakiwa ni matamshi yake ya moja kwa moja kuhusiana na suala hilo tangu aapishwe rasmi kushika madaraka. Katika mahojiano yaliyochapishwa na gazeti moja la Israel la Hayom Trump amesema anafikiria pia kwa umakini zaidi juu ya hatua ya kuuhamishia ubalozi wa Marekani mjini Jerusalem hatua ambayo imekuwa ikipingwa na Wapalestina ambao ndio wamiliki halali wa mji wa Jerusalem na miji mingine waliyodhulumiwa na Israel. Akizungumza na gazeti hilo ikiwa ni siku chache kabla ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu kuzuru Marekani wiki ijayo Trump amenukuliwa akisema kuwa yeye si mtu anayeamini kuendelea ujenzi wa makazi ya walowezi katika ardhi ya Wapalestina ni suala ambalo ni zuri katika mchakato wa kutafuta amani mashariki ya kati. Jumuiya ya kimataifa inaamini kuwa ujenzi wa makazi ya walowezi katika ukingo wa magharibi na Jerusalem mashariki ni kinyume cha sheria na unahatarisha matumaini ya kupatikana amani katika ukanda huo.

Mwisho wa habari/ 291


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky