Tuko bega kwa bega na taifa la Syria

Tuko bega kwa bega na taifa la Syria

Mmoja kati ya viongozi wa kikundi cha Hamasi amesema alipokuwa akizungumzia kuhusu ndege za kijeshi za Israel kushambulia Syria, amesisitiza kuwa Hamasi iko bega kwa bega na serikali ya Syria katika kukabiliana na majeshi ya kivamizi ya Israel

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kikundi cha mapambano ya kiislamu cha Hamasi, katika kukabiliana na mashambulizi ya majeshi ya utawala wa Israel nchini Syria, amesisitiza kuwa wananchi wa Palestina wako pamoja na Syria katika kukabiliana na uvamizi wa majeshi hayo ya utawala haramu wa Israel nchini Syria.
Hayo yamesemwa na Ismail Ridhwan, kiongozi mkuu wa kikundi cha Harakati ya Hamasi kuwa: tunaunga mkono majibu yaliotolewa na majeshi ya Syria dhidi ya majeshi ya anga ya Israel (kwa kuiangusha ndege ya kivita ya Israel nchini humo) na tunasisitiza kuwa Palestina iko bega kwa bega na serikali ya Syria katika kukabiliana na majeshi hayo vamizi.
Aidha yeye amepinga vikali mashambulizi ya kivamizi ya majeshi ya kizayuni katika ardhi ya Syria, na kusisitiza kuwa ni haki ya Syria kukabiliana na utawala huo kwa nguvu zote.
Kiongozi huyo wa Hamasi ameutaka Uma wa kiarabu na wananchi wa Palestina kukaa katika safu moja katika kukabiliana na vitisho vya utawala vamizi wa Israel kwa pamoja.
Inasemekana kuwa ndege za kivita za Israel asubuhi ya Jumamosi mara kadhaa ziliingia katika anga la Syria na kushambulia maeneo kadhaa ya maeneo ya mji wa Damascus nchini humo.
Mashambulizi na uvamizi huo ulikabiliwa na majibu ya kukta na shoka na kupelekea ndege mmoja ya Israel ya F16 kuripuliwa na kusambaratika kwa makombora ya anga ya majeshi ya Syria katika maeneo ya Golani.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky