Ufaransa yataka kuthibitiwa mbago wa makombora ya Iran

Ufaransa yataka kuthibitiwa mbago wa makombora ya Iran

Rais wa jamhuri ya Ufaransa amesema kuwa: tunapaswa kuichunguza na kuithibiti Iran kunako mpango wake wa makombora yake ya masafa marefu kwaajili ya kulinda usalama na amani ya ukanda wa mashariki ya kati

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: “Emmanuel Macron” Rais wa jamhuri ya Ufaransa ametaka kuchunguzwa mpango wa makombora ya masafa marefu ya serikali ya jamhuri ya kiislamu ya Iran.
Aidha katika maelezo yake kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran amesema: hakuna makubaliano mazuri yaliofikiwa kuhusu Iran zaidi ya makubalaino ya nyuklia ya Iran na kutokana na sababu hiyo, ndio maana Ufaransa ikawaq imesaini makubaliano hayo na hivi sasa inawataka wausika wa makubaliano hayo kuhifadhi mkataba huo.
Rais wa Ufaransa ameendelea kusema: sisi tunapaswa kuuchukunza ipasavyo mpango wa makombora ya masafa marefu ya Iran, kwaajili ya kulinda usalama na amani ya ukanda wa mashariki ya kati, aidha akiendelea kubainisha kuwa, makombora ya Iran yanatumika nchini Yemen na Syria, jambo ambalo linatishia amani na usalama washirika wetu katika ukanda wa mashariki ya kati.   
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky