Uhuru wa mwanadamu ni unatangulizwa kuliko kuikomboa nchi

Uhuru wa mwanadamu ni unatangulizwa kuliko kuikomboa nchi

Waziri mkuu wa Iraq amesema kuwa: kikundi cha kigaidi cha Daesh kimeharibu miundombinu na makazi ya wairaq, ama mwisho wa hayo yote Iraq ya sasa ni yenye mshikamano na imetoka na ushindi katika kukabiliana na Daesh

Shirika la habari AhlulBayt (a.s)  ABNA: “Haider Al-abadi” waziri mkuu wa Iraq ameyasema katika kongamano la kujadiliana kunako kuijenga upya Iraq amesema na kusisitiza kuwa Iraq inawakaribiasha wawekezaje kutoka nchi mbalimbali kuja kuwekeza nchini humo.
Aidha amebainisha kuwa: kurejea kwa wakimbizi katika makazi yao, ni baada ya kujengwa na kusawazisha miundombinu ya maeneo ya wakazi hao ambayo yaliokuwa yameharibiwa na kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini humo.
Aliendelea kusema: kutokana na kutokea hayo yote, hivi sasa Iraq imefikia ushindi mkubwa dhidi ya Daesh na kuifanya nchi hiyo kuwa na mshikamano zaidi ya awali, na kwa muono wetu kumkomboa mwanadamu ni kwenye kutangulizwa kuliko kuikomboa ardhi.
Waziri mkuu wa Iraq pia alibainisha masharti ya kuwekeza nchini Iraq na kusisitiza kwaajili ya kutoa usumbufu kwa wawekezaji serikali ya Iraq imeunda kamati maalumu ya kusimamia suala hilo.
Kongamano la kuijenga upya Iarq limefanyika leo nchini Kuwait likihudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu na wasimamizi wa masuala ya uchumi na baadhi ya viongozi wa Iraq ikiwemu kiongozi mkuu wa masuala ya kujenga upya maeneo yalikuwa yameharibiwa katika vita dhidi Ya Daesh nchini Iraq.
Kongamano hilo litaendelea kwa muda wa siku tatu, kongamano ambalo limehudhuriwa na majopo ya misafara sabini kutoka mataifa mbalimbali na ukanda wa mashariki ya kati.   
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky