Uingereza kuchukua hatua kali dhidi ya ugaidi

Uingereza kuchukua hatua kali dhidi ya ugaidi

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa ametowa wito wa kuwapo kwa hatua kali zaidi kupambana na makundi ya kigaidi kufuatia shambulio kwa kutumia gari na visu mjini London.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa  ametowa wito wa kuwapo kwa hatua kali zaidi kupambana na makundi ya kigaidi  kufuatia shambulio kwa kutumia gari na visu mjini London.

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa Jumapili ya leo tarehe 4 mwezi wa 6 mwaka 2017  ametowa wito wa kuwapo kwa hatua kali zaidi kupambana na magaidi kufuatia shambulio kwa kutumia gari na visu katika eneo la harakati mjini London na kutibua kampeni ya uchaguzi nchini Uingereza zikiwa zimebaki siku chache tu kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu huo.

Shambulio hilo lilianza na kumalizika haraka kwa polisi kuwauwa kwa kuwapiga risasi washambuliaji watatu katika muda usiozidi dakika nane.Lakini watu hao wametimiza lengo lao la kuugeuza usiku wa faraja mjini London kuwa wa balaa.

Shambulio hilo lilianza Jumamosi usiku wakati gari aina ya basi dogo lilipoacha njia na kungia katika njia ya wanaotembea kwa miguu katika daraja la London lenye harakati kubwa.Wanaume hao watatu walilikimbiza gari hilo wakiwa na visu vitatu vikubwa na kuwashambulia watu waliokuwa kwenye baa (vilabu vya pombe) na mikahawa karibu na soko la Borough kwa mujibu wa mashuhuda na polisi.

Maafisa wa huduma za dharura wamesema watu 48 wametibiwa katika hospitali za London wakiwemo wale waliokuwa na majeraha yenye kutishia uhai wao na wengine kadhaa waliokuwa hawakujeruhiwa sana. Idadi ya watu saba waliouwawa haijumuishi washambuliaji watatu.

Hilo ni shambulio la tatu kubwa kutokea nchini Uingereza katika kipindi cha miezi mitatu.Nchi hiyo tayari ilikuwa katika hali ya wasi kufuatia shambulio la bomu la kujitowa muhanga wiki mbili zilizopita katika onyesho la muziki wa Ariana Grande huko Manchester kaskazini magharibi mwa England ambalo limeuwa watu 22 na kujeruhi wengine wengi. Grande na wanamuziki wengine nyota Jumapili usiku walikuwa wakitarajiwa kupiga miziki wao katika onyesho la kuwachangia wahanga chini ya ulinzi mkali.

Makundi ya kigaidi yahusishwa

Kundi la kigaidi la Daesh linalojiita dola la Kiislamu lenye mafungamano ya karibu na Saudia arabia limedai kuhusika na mpripuko wa bomu wa Manchester lakini bado hakuna aliyedai kuhusika na shambulio hilo la London ambalo waziri mkuu amelihusisha na makundi  ya kigaidi.

May ambaye anakabiliwa na uchaguzi hapo Alhamisi amesema mashambulizi hayo ya hivi karibuni kabisa lilikiwemo lile lilitokea awali nje ya bunge hapo mwezi wa Machi hayahusiani moja kwa moja lakini "ugaidi huzaa ugaidi" na kwamba washambuliaji huwa wanaigizana . Amesema mashambulizi matano ya kuaminika yametibuliwa tokea mwezi wa Machi mwaka huu.

Amesema watu hao hunganishwa pamoja  na itikadi moja ya uovu itikadiya kigaidi ambayo huhubiri chuki, huchochea mgawanyiko na kuendeleza umadhehebu.

Amesema hiyo ni "itikadi inayodai kwamba maadili yetu ya kimagharibi na uhuru,demokrasia na haki za binaadamu hayaendani na dini ya Uislamu."

Kudhibiti mitandao

May ametowa wito kwa makampuni ya kimataifa ya mawasiliano kuchukuwa hatua zaidi za kuzuwia makundi ya itikadi kali kujipenyeza kwenye mitandao ambayo wanaitumia kuwaandikisha wanachama kwa kutumia maandishi ya siri kuhusu njama.

Waziri Mkuu amesema uchaguzi utafanyika kama ulivyopangwa.Vyama vikuu vilistisha kampeni za uchaguzi Jumapili kutowa heshima kwa wahanga juu ya kwamba chama cha UK Independence kimesema kitaendelea na kampeni kuwaonyesha watu wenye itikadi kali hawawezi kuikengeuka demokrasia.

Chama cha Conservative cha May kilikuwa kikitegemewa kupata ushundi wa tofauti jubwa ya kura lakini uchunguzi wa maoni wa hivi karibuni umeonyesha mchuano unazidi kuwa mkali.Haijulikani vipi matumizi hayo ya nguvu yasio kifani yanaweza kuwa na taathira kwa hisia za wapiga kura.

Kwa bahati mbaya uingereza ni moja kati ya mataifa yanayounga mkono upande wa magaidi nchini Syria na inahisa kubwa katika kusambaa magaidi hao.

Mwisho wa habari / 291

 

 


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky