Uingereza, Ujerumani na Ufaransa zakubali kufanya biashara na Iran bila ya kutumia Dola

Uingereza, Ujerumani na Ufaransa zakubali kufanya biashara na Iran bila ya kutumia Dola

Kwa mujibu wa maelezo ya waziri wa mambo ya nje wa Urusi: kufanya biashara na Iran “bila ya kutumia Dola” kutatoa athari nzuri na kuwafaididha wafanya biashara na kampuni ndogondo na saizi ya kati zinazotaka kufanya biashara na Iran

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: hayo yamesemwa na Sergey Lavrov waziri wa mambo ya nje wa Urusi na kutangaza kuwa nchi tatu za Ulaya zimekubali kuendelea kukuza fungamano lake la kibiashara na Iran bila ya kutumia Dola ya kimarekani.
Aidha alisema siku ya Jumatatu kuwa nchi tatu za Ulaya “Ujerumani, Ufaransa na Uingereza” kwa itaendelea kufanya biashara na Iran bila kutumia Dola, pia kwa mujibu wa maelezo ya Lavrov ni kwamba maamuzi hayo yatawanufaisha wafanya biashara wadogowadogo na kampuni za saizi ya katika ambazo zilikuwa na matumaini makubwa ya kufanya biashara na Iran.
Mwisho amemalizaia kwa kusema kuwa: wajumbe wa makumbaliano ya mpango wa Nyuklia wa Iran wameafikiana kupanga mpango kazi wa kuzuia vikwazo vya Marekani visiathiri katika mashirika na uchumi wa Iran.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky