Ujerumani na Ufaransa zataka haki za magaidi zihifadhiwe katika mzozo wa Syria

Ujerumani na Ufaransa zataka haki za magaidi zihifadhiwe katika mzozo wa Syria

Trump anaamini kwamba kuondolewa madarakani Bashar assad itakuwa ni kosa kama kosa lililofanyika kumuondoa Gaddafi Madarakani ambapo msimamo huo unatofautiana kabisa na msimamo wa Obama.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Mawaziri wa mambo nya nje wa Ujerumani na Ufaransa hawakuweka matumaini makubwa ya kupatikana kwa ufumbuzi katika mazungumzo ya amani yaliopangwa kufanyika Geneva wiki ijayo kukomesha vita vya miaka sita Syria kama magaidi hawatapewa haki zao.

"Mazungumzo ya leo yalikuwa muhimu kuratibu hatua zetu kwa sababu tunataraji kuingia katika mchakato mpya wa kisiasa kwa kuanza upya mazungumzo mjini Geneva lakini wakati huo huo pia tunahitaji kuzingatia uhalisia. Hili pia limekuja kudhihirika"

Hiyo ni kauli ya Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani  Sigmar Gabriel wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliohudhuriwa pia na waziri mwenzake wa Ufaransa Jean- Marc Ayrault mjini Bonn kufuatia mazungumzo na nchi nyengine wanachama wa kundi lilolojilikana kama Marafiki wa Syria pembezoni mwa mkutano wa kundi la mataifa 20 yenye maendeleo makubwa ya viwanda na yale yenye kuinukia kiuchumi.

Mawaziri hao wametahadharisha kwamba wasidharau ugumu na hatari ilioko na kwamba hakuna makubaliano yaliofikiwa. Mawaziri hao pia wametowa wito kwa Urusi kutimiza dhima yenye tija katika juhudi za kukomesha vita hivyo vya miaka sita ambavyo zinachochewa na magaidi wanaodhaminiwa na Marekani na washirika wake kutoka nchi 61.

Pia wameitaka Urusi pamoja na Iran kufahamu uhalali wa magaidi wa Syria kama wapinzani ili kuruhusu wawakilishi wa upinzani kuwa na dhima kubwa katika mazungumzo hayo ya amani yanayodhaminiwa na Umoja wa Mataifa.

Wawakilishi wa utawala wa Rais Bashar al Assad wa Syria na makundi ya upinzani wameshindwa kufikia ufumbuzi katika mazungumzo yaliofanyika wiki hii katika mji mkuu wa Kazakhstan Astana kutokana na ushawishi kutoka nchi za nje.

Fursa kujua msimamo wa serikali ya Trump

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Jean- Marc Ayrault amesema kuchaguliwa kwa serikali mpya ya Marekani kumetowa fursa kutathmini mchakato huo wa kutafuta njia za kukomesha mzozo huo wa Syria ambapo Umoja wa Mataifa umesema umeuwa takriban watu 400,000.

Ayrault amesema "Ni wiki chache tokea kundi hili lilipokutana kwa mara ya mwisho na limekuwa jambo muhimu kwetu baada ya kupatikana kwa serikali mpya nchini Marekani ilikuwa ni fursa kwetu kubadilishana mawazo na mwezetu Rex Tillerson .Nafikiri ni muhimu na kitu chenye kufaa kabisa kuwa na mazungumzo ya karibu na Marekani juu ya suala la Syria na masuala mengine mengi."

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson amebanwa akitakiwa aelezee kwa ufasaha msimamo wa Marekani juu ya mzozo huo wa Syria kabla ya kuanza kwa mazungumzo ya Geneva.

Tillerson katika safari yake ya kwanza ya kidiplomasia nchi za nje anakabiliwa na shinikizo la kuelezea msimamo wa Trump juu ya hatima ya Rais Bashar al Assad.

Trump anaamini kwamba kuondolewa madarakani Bashar assad itakuwa ni kosa kama kosa lililofanyika kumuondoa Gaddafi Madarakani ambapo msimamo huo unatofautiana kabisa na msimamo wa Obama.

Mwisho wa habari/ 291


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky