Ujerumani, Ufaransa na Uingereza zasisitiza kushikamana na makubaliano ya Nyuklia ya Iran bila ya Marekani

Ujerumani, Ufaransa na Uingereza zasisitiza kushikamana na makubaliano ya Nyuklia ya Iran bila ya Marekani

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, Ufaransa na Uingereza wamesisitiza kubaki kwako katika makubaliano ya mpango wa Nyuklia ya Iran, hata kama Marekani itajivua katika makubaliano hayo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: hayo yamesemwa na waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa alipokuwa akitoa kauli ya pamoja ya mataifa matatu ambazo ni Ufaransa, Ujerumani na Uingera, amebainisha kuwa kama Marekani itajitoa katika makubaliano ya mpango wa nyuklia wa Iran wao watabaki chini ya mkataba huo.
Kadhalika waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani pia amebainisha kuwa, nchi yake itaendelea kubaki katika makubaliano ya mpango wa Nyuklia wa Iran hata kama Rais wa Marekani atajitoa katika makubaliano hayo.
Aidha amesisistiza kuwa: watafanya kila liwezekanalo kwaajili ya kubaki kwa makubaliano baada ya tarehe 12 mwei Mei mwaka huu, tarehe ambayo marekani imetangaza kuwa itajitoan katika makuvaliano ya mpango wa nyuklia wa Iran yalifanywa na kikundi cha 5+1 mwaka 2015.
Naye alibainisha kuwa: pamoja na hayo yote bado tunasubiri maamuzi ya Marekani kushusu makubaliano hayo tuone kuwa atajitoa au atabaki, ama kwa mtazamo wetu, hakuna njia yeyote bora zaidi kinyume na kuhifadhi na kushikamana makubaliano hayo, kwani kwa kufanya hivyo tutaweza kuzuia kwa kiasi fulani harakati za masuala ya Nyuklia ya Iran.
Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa amesema alipokuwa na waandishi wa habari katika mji mkuu wa Ujerumani na kusisitiza kuwa: Ufaransa, Ujerumani na Uingereza, tumekubaliana kubaki katika makubaliano ya mpango wa Nyukilia wa Iran kwani hiyo ndio njia pekee itakayoifanya Iran isiweze kumiliki silaha za nyuklia.
Hivi mwishoni Rais wa Ufaransa alkadhalika Angela Merkel kiongozi mkuu wa Ujerumani walikwenda nchini Marekani na kuonana na Trump kwaajili ya kumtaka abaki katika makubaliano hayo. Huku habari za hivi punde zinaashiria kuwepo safari ya waziri wa mambo ya nje wa Uingereza kwenda nchini Marekani kwaajili ya kumtaka Rais wa Marekani aendelee kubaki katika makubaliano hayo.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky