Ujerumani yawafukuza wanadiplomasia

Ujerumani yawafukuza   wanadiplomasia

Marekani imeunga mkono, kwa haraka hatua iliyochukuliwa na baadhi ya nchi za Ulaya kwa kuwafukuza wanadiplomasia 60 wa Urusi kutoka ndani ya mipaka yake.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Ujerumani na nchi nyingine za Ulaya zimewafukuza wanadiplomasia wa Urusi kutokana na mkasa wa kupewa sumu mpelelezi wa zamani wa Urusi na binti yake huko nchini Uingereza ambako hadi sasa wamo katika hali mahututi.

Wizara ya Mambo ya nje ya Ujerumani imesema itawafukuza wanadiplomasia wanne wa Urusi kwa sababu ya madai hayo ya kupewa sumu mpelelezi wa zamani wa Urusi Sergei Skripal na binti yake Yulia. Nchi kadhaa za magharibi zimetangaza pia kwamba zitachukua hatua za kali dhidi ya Urusi.Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas ameaandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba Urusi lazima itoe maelezo kuhusu shambulio hilo la Salisbury na wakatim huo huo amesema kwamba hatua ya Ujerumani ni kuonyesha kwamba inasimama pamoja na Uingereza.

Rais wa Tume ya Ulaya Donald Tusk amesema nchi 14 za Umoja wa Ulaya, zikiwa ni pamoja na Ufaransa, Poland, na mataifa ya Baltic yatachukua hatua za kuwafukuza wanadiplomasia wa Urusi nchini mwao.

Hatua za ziada, ikiwa ni pamoja na kufukuzwa Urusi kutoka kwenye mfumo wa kawaida wa Umoja wa Ulaya, zitazingatiwa katika siku na wiki zijazo amesema bwana Tusk.

Marekani imeunga mkono, kwa haraka hatua iliyochukuliwa na baadhi ya nchi za Ulaya kwa kuwafukuza wanadiplomasia 60 wa Urusi kutoka ndani ya mipaka yake.

Balozi wa Urusi nchini Marekani Anatoly Antonov amesema uamuzi wa Washington wa kuwafukuza wanadiplomasia wake 60 unaharibu kile kilichobaki katika mahusiano kati ya Urusi na Marekani.

Msemaji wa serikali ya Urusi Dmitry Peskov amesema kanuni ya usawa itafanya kazi katika kila tukio na ameahidi kwamba Urusi italipiza kisasi kwa kila hatua itayofanywa dhidi yake.

Uingereza tayari imewaamuru wanadiplomasia 23 wa Urusi kuondoka nchini humo, hatua ambayo itachochea hatua za kulipiza kisasi kwa kufukuzwa wafanyakazi wa kidiplomasia wa Uingereza kutoka mjini Moscow. Umoja wa Ulaya tayari umemwamuru balozi wake wa nchini Urusi  aondoke.

Mnamo Machi 4, Sergei na Yulia Skripal walikutwa wakiwa mahututi katika bustani ya huko Salisbury, Uingereza, ambapo Skripal ameishi tangu alipoachiwa kutoka jela mnamo mwaka 2010 kufuatia mpango wa kubadilishana wafungwa na Marekani. Watu hao wawili baba na binti yake bado wamo katika hali mahututi kwenye hospitali moja nchini Uingereza.

Urusi imekanusha kabisa  kuhusika na madai ya kupewa sumu watu hao wawili na kuomba ushahidi utolewe lakini Uingireza imeshindwa kutoa ushahidi madhubuti. Mwiso wa habari/ 291

 


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky