Umoja wa mataifa: Iran haitumi misaada ya silaha nchini Yemen

Umoja wa mataifa: Iran haitumi misaada ya silaha nchini Yemen

Kwa mujibu wa ripoti ya wataalamu wa Jumuia ya umoja wa mataifa, ni kwamba serikali ya Jamhuri ya kiislamu ya Iran mpaka sasa haijakiuka maamuzi ya 2231 ya jumuia hiyo, yaliokuwa na dhumuni la kuwa Jamhuri ya kiislamu ya Iran hairuhusiwi kutuma tuma silaha nchini Yemen

Shirika la habari AhlulaBayt (a.s) ABNA: hii ni katika hali ambayo serikali ya Marekani ikishirikiana na baadhi ya wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa, daima wamekuwa wakidai kuwa jamhuri ya kiislamu ya Iran imekiuka maamuzi ya Umoja wa Mataifa ya 2231, yanayo husu kuzuiliwa kwa jamhuri ya kiislamu ya Iran kutuma silaha nchini Yemen.
Ama hivi karibuni Baraza la usalama la Umoja wa mataifa lilikuwa na kikao cha siri, ambapo katika kikao hicho kwa mujibu wa ripoti za wataalamu wa masuala hayo, wamesema kuwa: hakuna ilama inayoashiria kuwa, meli ziliokuwa zimesitishwa kwa madai kuwa zinasilaha za Iran zinazokwenda Yemen, haijaonekana silaha yoyote ya Iran pia hata kufahamika kuwa silaha hizo zimechukuliwa Iran.
Chanzo kimoja katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa baada ya kutangaza habari hii amesema kuwa “Saudi Arabia haijaridhishwa na ripoti hiyo na inafanya juhudi kuwa, ripoti hiyo isifikishwe rasmi katika Jumuia ya Umoja wa mataifa ikiwa kama sanadi na kithibitisho cha madai hayo”.    
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky