Umoja wa Mataifa Kuangamiza kwa jamii ya kiislam nchini Myanmar kunaendelea

Umoja wa Mataifa Kuangamiza kwa jamii ya kiislam nchini Myanmar kunaendelea

Kwa mujibu wa maelezo ya viongozi wa umoja wa mataifa ni kwamba: majeshi ya Myanmar yanaendeleza mpango wake wa kuwasambaratisha waislamu wa nchi hiyo na kwa kuwauwa au kuwalazimisha kukimbilia nchini Bangladesh

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: mmoja kati ya viongozi wakuu wa jumuia ya umoja wa Mataifa amesema kuwa mpango wa kuisambaratisha jamii ya kiislamu nchini Myanmar bado unaendelea nchini humo.
Kwa majibu wa maelezo yake majeshi ya Myanmar yanatumia mbalimbali wakitaka za kuisambaratisha jamii hiyo ikiwemo kuwawekea vikwazo mbalimbali ikiwemo kuwalazimisha kuondoka nchini humo na kwenda nchi jirani ya Bangladesh.
Toka mwaka uliopita mpaka sasa watu zaidi ya laki saba ambao ni wakazi wa Rohingya wakimbilia nchini Bangladesh, ambapo jumuia ya umoja wa Mataifa hulitaja suala hilo kuwa ni mpango wa kuifuta jamii hiyo katika taifa hilo.
Aidha kiongozi huyo ambaye ni msimamizi wa masuala ya haki za binadamu baada ya kuikosoa vitendo vya serikali na majeshi ya Myanmar akisema na kubainisha kuwa mienendo ya serikali hiyo haifahami kwa sababu haionyeshi msimamo mmoja, ambapo baadhi ya mida huwadai wananchi wake wote waliokimbilia nchini Bangladesh kurudi katika mazi yao, ama kwa upande mwingine majeshi ya taifa hilo huwalazimisha wakazi waisalmu waliopo ndani ya taifa kuendelea kuwafukuza na kuwataka wakimbilie nchini Bangladesh.
Mwisho alimazia kwa kusema kuwa mpango huo wa  kusambaratisha jamii ya waislamu, jeshi la nchi hiyo ndio linaofanya kazi hiyo, ama serikali ndio inayotowa msukumo wa kufanywa kwa jambo hilo.
Kwa upande mwingine majeshi ya Myanmar yamedai kuwa, mauaji yaliofanyika katika ya mwaka uliopita kupitia majeshi hayo, ilikuwa ni kujibu mashambulizi ya vikundi vilivukuwa na silaha viliokuwa vinatishia usalama wa taifa hilo katika sehemu hiyo.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky