Umoja wa mataifa: mpaka sasa watu 923 wafariki dunia kwa ugonjwa wa kipindupindu nchini Yemen

Umoja wa mataifa: mpaka sasa watu 923 wafariki dunia kwa ugonjwa wa kipindupindu nchini Yemen

Jumuia ya umoja wa mataifa imetoa ripoti yakuwa kila dakika ipitapo mtu mmoja hulazwa katika hospitali kwa ugonjwa wa kipindupindu katika mahospitali ya nchi hiyo, huku ikitoa angalizo la kunea kwa ugonjwa huo nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Jumuia ya Umoja wa mataifa imetoa takwimu mpya inayoashiria kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu, ampapo mpaka sasa  watu wapatao 923 wamepoteza maisha katika watu laki moja na ishirini na tatu elfu, walikuwa wamepatwa na ugonjwa huo nchini humo.
Shirika la habari la Ufaransa limetangaza kutoka mji mkuu wa Yemen, kuwa jumuia ya umoja wa mataifa imetoa taarifa kuwa kila inapopita dakika moja mtu mmoja huwasilisha hospitali na kulazwa kwakupatwa na ugonjwa kipindupindu katika mahospitali ya nchi hiyo.
Mpaka hivi sasa viongozi wa Hospitali y Sabin wamelazimika kutengeza mahema ya kuwalaza wagonjwa hao kutokana na nafasi ya hospitali hiyo kutotosha, hivyo wagonjwa watalazwa katika mahema hayo yaliofungwa pembeni mwa hospitali hiyo kwa muda.
Aidha viongozi wa hospitali hiyo wameshiria kuwepo na mapongufu ya vitendea kazi muhimu ikiwemo madawa, vitanda na vinginevyo, haliyakuwa kila baada ya muda wagonjwa wa kipindupindu wazidi kuwa wengi katika sehemu hiyo.
Kusambaa kwa ugunjwa huo kumesababishwa na mgomo wasimamizi wa usafishaji wa mazingira ikiwemu wakusanyaji uchafu katika mji mkuu wa nchi hiyo kwakile walichodadi kuwa hawajapewa mishahara kwa muda mrefu.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky