Umoja wa Mataifa: ukame wahatarisha maisha ya watoto milioni 13 nchini Yemen

Umoja wa Mataifa: ukame wahatarisha maisha ya watoto milioni 13 nchini Yemen

Mwakilishi wa jumuia ya umoja wa Mataifa nchini Yemen amesema: kuendelea kwa vita nchini Yemen kutapelekea kuhatarika zaidi maisha ya watoto waliopo nchini humo kwa ukame

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: jumuia ya Umoja wa Mataifa imetoa tamko la kutahadharisha kuwa uchache wa chakula nchini humo unahatarisha maiasha ya wato zaidi ya milioni 13 nchini humo.
Hayo yamesemwa na mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen na kusisitiza kuwa, kama vita itakuwa yenye kuendelea nchini Yemen, itapelekea kupatikana kwa ukame mkubwa nchini humo, huku akibainisha kuwa kutokana na yale yanayojiri hivi sasa nchini jumuia za kimataifa zinapaswa kuona haya kwa hilo.
Aidha kwa upande mwengine Jumuia ya Umoja wa Mataifa umeutaka umoja ulioivamia Yemen chini ya usimamizi wa Saudi Arabia kuacha kufanya mashambulio ya anga ambayo kwamba yanasababisha kukwamisha maisha ya wananchi wasiokuwa na hatia, mashambulio ambayo husambaratisha masoko maospitali hata sehemu za masomo.
Vita dhidi ya Yemen ilianza mnamo miaka mitatu iliopita ambapo mpaka sasa watu zaidi elfu 10 wameuwawa na wengine wengi kujeruhiwa na wengine kuwa wakimbizi na kukimbia nchi yao, ama ripoti zinaashiria kuwa idadi kubwa ya waliopoteza maisha katika vita hiyo ni wananchi wa kawadi wakiwemo watoto.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky