Umoja wa mataifa walaani vikali mauaji yanayofanywa na Saudia nchini Yemen

Umoja wa mataifa walaani vikali mauaji yanayofanywa na Saudia nchini  Yemen

Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wamesema Saudia arabia na washirika wake nchini huenda zimehusika katika uhalifu wa kivita dhidi ya wananchi madhulumu wa Yemen, wakitaja mashambulizi makali ya anga, udhalilishaji wa kingono na watoto kutumikishwa kama wapiganaji.

Shirika la habari la ABNA linaripotikuwa: Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wamesema Saudia arabia na washirika wake nchini huenda zimehusika katika uhalifu wa kivita dhidi ya wananchi madhulumu wa Yemen, wakitaja mashambulizi makali ya anga, udhalilishaji wa kingono na watoto kutumikishwa kama wapiganaji.

Katika ripoti yao ya kwanza, kundi la wachunguzi wa Umoja wa Mataifa limesema kuna ushahidi wa kutosha kudhihirisha kuwa wanaohusika katika mzozo wa Yemen, wamekiuka sheria za kimataifa kuhusu haki za binadamu.

Mzozo huo wa Yemen, ambayo ni mojawapo ya nchi masikini zaidi duniani, umesababisha kile Umoja wa Mataifa ulichokiita mojawapo ya migogoro mibaya zaidi ya kibinadamu duniani. Ambapo saudia arabia na washirika wake ikisaidiwa na Marekani, Ufaransa, Uingereza  na Israel wamekuwa wakifanya mashambulizi makali ya kinyama dhidi ya raia wasio na hatia wa Yemen.

Raia ndiyo waathiriwa wakubwa

Mapema leo, Misururu ya mashambulizi makali ya angani yameripotiwa kulenga uwanja wa ndege wa kimataifa wa Yemen ulioko katika mji mkuu Sanaa, unaodhibitiwa na waasi na kambi ya jeshi la angani iliyoko mkabala na uwanja huo wa ndege. Waasi wa Houthi wanawaulumu wanajeshi wa serikali kwa mashambulizi hayo.

Mashambulizi hayo yaliyoulenga uwanja huo wa ndege ambao hautumiki sana isipokuwa na ndege za Umoja wa Mataifa na kambi ya kijeshi ya Al Dailami yanakuja saa chache baada ya Wahouthi kusema wameulenga uwanja wa ndege wa Dubai kwa shambulizi la ndege isioendeshwa na rubani. Saudi Arabia imesema imenasa kombora lililorushwa na waasi wa Houthi katika jimbo la Najran.

Hayo yanaripotiwa wakati ambapo Umoja wa Mataifa unapanga mkutano wa kutafuta amani kati ya serikali ya Yemen na waasi wa Houthi utakaofanyika tarehe 6 mwezi ujao mjini Geneva.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa inaangazia ukiukwaji wa haki za binadamu kuanzia mwezi Septemba mwaka 2014 hadi mwezi Juni mwaka huu, hivyo haiangazii mlolongo wa mashambulizi ya siku za hivi karibuni ambayo yamewaua watoto wengi wanaoishi katika maeneo ya kiraia. Mashambulizi hayo yamelaaniwa vikali na Jumuiya ya Kimatiafa.

Muungano huo wa kijeshi haujakanusha au kuthibitisha kufanya mashambulizi mawili ya anga Alhamisi iliyopita ambayo Umoja wa Mataifa umesema yamewaua takriban watoto 50 na wanawake wanne kusini mwa mji wa Hodeida.

Vita vya Yemen vimesababisha vifo vya zaiadi ya watu 10,000 wengi wakiwa ni wanawake, watoto na raia wasio na hatia.

Hata hivyo mwanamfalme wa Saudia arabia amesikika akisema wataendeleza mashambulizi makali dhidi ya Yemen mpaka wananchi wayemen wapate hofu kila wanaposikia jina la Saudia arabia.

Mwisho wa habari/ 291

 


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky