UNICEF: kila dakika 10 mtoto mmoja hufariki nchini Yemen

UNICEF: kila dakika 10 mtoto mmoja hufariki nchini Yemen

Mmoja kati ya viongozi wa shirika la UNICEF amesema kuwa: katika kila dakika 10 mtoto mmoja hufariki nchini Yemen kufuatia kuzingirwa na kuendelea kwa vita na njaa na magonjwa.

Shirika habari la Habari AhlulBayt (a.s) ABNA: msimamizi wa washirika la kusaidia watoto duniani UNICEF: amebainisha kuwa watoto walikuwa wamezingirwa nchini Yemen, kufuatia hali hiyo kila katika dakika kumi mtoto mmoja hupoteza maisha kwa njaa na maradhi.
Aidha kiongozi huyo amebainisha kuwa: shirika hilo limeomba kiasi cha Dola milioni miatatu na hamsini kwaajili ya kuwasaidia watoto hao, huku akisistiza kuwapesa hiyo ukilinganisha na zile zinazo nunuliwa silaha dhidi ya wanadamu ni chache mno.
Kwa upande mwingi amesema kuwa: pande zote mbili za malumbano nchini Yemen hazizingatii haki za watoto katika vita nchini humo.
Siku ya Jumapili Shirika la UNICEF limesisitiza kuwa bajeti iliokuwa nayo haitosheleza katika kuwasaidia walioadhirika na vita hiyo nchini humo, huku akibainisha kuwa kwa sasa tunahitaji Dola milioni 350 za haraka kwaajili ya kukuza misaada ya kibinadamu hitajika nchini humo.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky