UNICEF: Tani elfu 50 za misaada zawasili bandari ya Al-hudaidah Yemen

UNICEF: Tani elfu 50 za misaada zawasili bandari ya Al-hudaidah Yemen

Shirika la vyakula duniani limetoa taarifa ya kuwasili misaada ya kibinamu ambazo ni tani elfu 50 za vyakula na kushuhswa katika Bandari ya Alhudaidah nchini Yemen

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: UNICEF imetangaza siku ya Jumapili katika kauli yake kuwa tani elfu 50 za vyakula zimewasili katika Bandari ya Al-hudaidah iliopo magaharibi mwa Yemen.
Alkadhalika meli ya Uturuki iliobeba ngano na imewasili katika Bandari ya As-swalif ambayo pia ipo katika sehemu ya Al-hudaidah, kwa upande mwingi umoja wa falme za kiarabu leo imetangaza kusitisha mapambano yaliokuwa yanaendelea katika sehemu ya Al-hudaidah.
Aidha waziri mshauri wa serikali ya Falme za Kiarabu katika mambo ya kimataifa, amedai kuwa sababu ya kusiitisha mapigano hayo kwaajili ya hatua ya kuwasilisha misaada ya kibinadamu chini ya usimamizi wa umoja wa mataifa na kufanya juhudi za kuleta suluhu.
Msimamizi wa mashariki ya kati na kaskazini mwa Afrika ndani ya UNICEF ametangaza takriban watoto milioni mbili wa Yemen wamepatwa na madhari kufuatia kuwa na lishe mbaya na zaidi ya watoto milio 11 wa Yemen wanahitaji msaada wa chakula.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky