Upinzani wa Syria wasusia mazungumzo ya amani

Upinzani wa Syria wasusia mazungumzo ya amani

Duru ya tatu ya mazungumzo ya amani ya Syria ambayo ilitarajiwa kuanza leo katika mji mkuu wa Kazakhstan- Astana imekwama, baada ya kususiwa na upande wa magaidi unaoungwa mkono na Uturuki na washirika wake. Upinzani umeituhumu Urusi na serikali ya Rais Bashar al-Assad, kwa uhalifu kuhusiana na kile kinachoendelea nchini Syria.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Duru ya tatu ya mazungumzo ya amani ya Syria ambayo ilitarajiwa kuanza leo katika mji mkuu wa Kazakhstan- Astana imekwama, baada ya kususiwa na upande wa magaidi  unaoungwa mkono na Uturuki na washirika wake. Upinzani umeituhumu Urusi na serikali ya Rais Bashar al-Assad, kwa uhalifu kuhusiana na kile kinachoendelea nchini Syria. Urusi kwa upande wake imesema sababu zilizotolewa na upinzani haziridhishi wala hazina mashiko, na kuongeza kuwa uamuzi huo umekuja kwa kushtukiza. Upinzani umetangaza leo hii kuwa usingeshiriki katika mazungumzo hayo, ukiilaumu Urusi kwa kukataa kusitisha mashambulizi ya anga katika maeneo yanayodhibitiwa na magaidi, na kushindwa kuwashawishi wanajeshi wa serikali na wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran, kuheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano.

Serikali ya Syria pia inawalaumu magaidi hao ambao inawaita kuwa ni vibaraka wa Uturuki, na kusema Uturuki imeshindwa kutimiza wajibu wake kuhusu mchakato wa amani wa Astana, kwani magaidi hao wameendelea kutesa wananchi na kudhulumu mali za umma. Mazungumzo hayo hudhaminiwa na Urusi, Uturuki na Iran.

Mwisho wa habari/ 291

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky