Urusi: Marekani imekurupuka kuhusu ghasia za Iran

Urusi: Marekani imekurupuka kuhusu ghasia za Iran

Baada ya Marekani na washirika wake, kuunga mkono waandamanaji wanaopinga serikali ya Iran, na kuitisha kikao cha dharura kuhusu hali ya Iran....

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Baada ya Marekani na washirika wake, kuunga mkono waandamanaji wanaopinga serikali ya Iran, na kuitisha kikao cha dharura kuhusu hali ya Iran. Serikali ya Iran imeuambia Umoja wa Mataifa inao ushahidi kwamba maandamano ya upinzani yaliyotokea nchini humo yameratibiwa kutoka nje, na Urusi imelitaka Baraza la Usalama kuiacha Iran ishughulikie yenyewe masuala yake ya ndani bila ya kuingiliwa na mataifa ya nje.

Marekani ambayo imejingiza kwenye mgogoro huo,  kwa upande wake imesema Iran isije ikasema haijatahadharishwa.

Hayo yalijiri katika kikao cha dharura cha Baraza la Usalama mjini New York ambacho kiliitishwa na Marekani jana Ijumaa, kujadili wimbi la maandamano ambalo liliitikisa Iran wiki iliyopita. Kikao hicho kilianzia faraghani, lakini baadaye Marekani ilifanikiwa kukifanya cha wazi licha ya upinzani kutoka Urusi, Ufaransa, Bolivia na wanachama wengine wengi.

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley alitoa hoja kwamba maandamano hayo ya Iran, kwanza yale ya kuipinga serikali na baadaye yale ya kuinga mkono, yanaweza kuitumbukia nchi hiyo katika mzozo wa vita mithili ya ile ya Syria. ''Uhuru na heshima ya binadamu haviwezi kutenganishwa na amani na usalama'', alisema Bi Haley. Balozi huyo wa Marekani aliitahadharisha Iran, akisema dunia inafuatilia yanayofanyika.

Marekani ilitamani kuona machafuko yanatokea nchini Iran lakini njama zao zimegonga mwamba, baada ya serikali ya Iran kuzuia maandamano  hayo, ambayo kimsingi hayakuwa makubwa lakini yalikuzwa na vyombo vya habari kwa lengo la kuharibu.

Trump apigia aahidi kusaidia waasi wa serikali  ya Iran

Rais wa Marekani baada ya kusikika akihamasisha uasi nchini Iran kwasasa ameajizuia kuhimiza ghasia na vitendo vya fujo kwa waandamanaji wa upinzani nchini Iran, lakini alielezea heshima kwa kile alichokiita ''juhudi za watu wa Iran za kutaka kudhibiti tena serikali yao'' aliyoitaja kuwa ya kifisadi. Hali kadhalika Trump aliahidi msaada wa Marekani kwa waandamanaji hao kwa wakati wowote muafaka.

Gholamali Khoshroo, balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa aliliambia baraza kuwa serikali ya nchi yake inao ushahidi wa dhahiri kwamba maandamano ya kupinga serikali yalikuwa yakiongozwa kutoka nje, na aliishutumu Marekani na washirika wake kutumia vibaya nafasi yake kama mwanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kuitisha kikao hicho cha dharura cha kujadili maandamano nchini Iran.

Urusi na Ufaransa pia zilikuwa zimehoji umuhimu wa kuitisha kikao hicho kwa pupa.  Na kuilaumu serikali ya Marekani kwa kukurupuka katika suala la Iran, Balozi wa Ufaransa Francois Delattre alisema ingawa aligutushwa na ghasia iliyoshuhudiwa katika mitaa ya miji ya Iran, matukio hayo hayakuwa kitisho kwa usalama na utengamano wa kimataifa, hadi yafikishwe mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Ufaransa yatoa Onyo kwa wanaotaka kujinufaisha na mzozo wa Iran

Delattre alisema, ''Ni lazima tuwe makini sana na wanaoazimia kuutumia mzozo huu kwa maslahi yao binafsi'', na kuongeza kuwa dunia inapaswa kuendelea kufuatilia hali hiyo kwa karibu.

Marekani na Saudia arabia zilionekana kushawishi raia wa Iran kwa hali na Mali ili wafanye fujo na maandamano ya ghasia lakini weledi wa wananchi na viongozi wa Iran ulizuia hatua hiyo na kuwaacha maadui wakiwa vinywa wazi.

Mtazamo wa Ufaransa uliungwa mkono na mwenzake wa Urusi Vassily Nebenzia, ambaye alisema pamoja na kusikitishwa na maafa yaliyotokea, bado Iran inapaswa kuachwa kushughulikia matatizo yake ya ndani.

Awali naibu waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Rybakov, aliishutumu Marekani kukosa aibu katika kujiingiza katika maandamano ya Iran ambayo alisema ni masuala ya ndani kabisa ya nchi hiyo.

Maandamano hayo ya upinzani nchini Iran yaliyoanzia katika mji wa Mashhad ambao ni wa pili kwa ukubwa nchini humo, yalisababisha vifo vya watu kadhaa waliojaribu kuvamia kituo cha polisi ili kutwaa silaha. Mamia wengine waliwekwa kizuizini. Kwa sasa kuna maandamano kama ya Iran nchini Saudia arabia ambapo wananchi wanadai demokrasia na ugumu wa maisha, suali ni kwamba je vyombo vya habari vitalitangaza na kuzikuza tukio hilo kama ilivyokuwa kwa Iran, na Je Marekani itakuwa upande wa wananchi wa Saudia arabia?.

Mwisho wa habari / 291

 


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky