Urusi na China zapinga vikwazo vya kidhalimu dhidi ya Syria

Urusi na China zapinga vikwazo vya kidhalimu dhidi ya Syria

Urusi na China ambazo zinaunga mkono serikali ya Syria zimepinga kuiwekea Syria vikwazo vya Umoja wa Mataifa kupitia kura ya turufu. Urusi imesema hakuna ushahidi wa kutosha wa kufanya hivyo. Marekani ambayo inasaidia magaidi nchini Syria imelaani vikali hatua hiyo ya Urusi na China.

Shirika la habari la  ABNA linaripoti kuwa: Urusi na China ambazo zinaunga mkono serikali ya Syria zimepinga kuiwekea Syria vikwazo vya Umoja wa Mataifa kupitia kura ya turufu. Urusi imesema hakuna ushahidi wa kutosha wa kufanya hivyo. Marekani ambayo inasaidia magaidi nchini Syria imelaani vikali hatua hiyo ya Urusi na China.

Uchunguzi wa pamoja kati ya Umoja wa Mataifa pamoja na shirika la kufuatilia utumiaji wa silaha za kemikali umedhihirisha kuwa, serikali ya Syria ilifanya mashambuluzi matatu ya kutumia gesi ya klorini na wanamgambo wa kundi la kigaidi la Daesh wanaodhaminiwa na Saudia arabia wamefanya shambulio moja la kutumia gesi ya haradali. Balozi wa Marekani kwa umoja huo, Nikki Haley, amezituhumu nchi zote mbili kwa kushindwa kuiwajibisha serikali ya Rais wa Syria Bashar al-Asaad kwa kutumia silaha za kemikali hata baada ya uchunguzi kuthibitisha.

"Uchunguzi uliofanywa hauna tatizo lolote. Urusi haitaki tu kuukosoa utawala wa Assad kwa kosa la kutumia silaha za kemikali. Huo ndiyo ukweli. Kwa hiyo ujumbe gani tunauonesha ulimwengu? Ukiwa mshirika wa China na Urusi watawatetea marafiki zao hata ambao wanatumia silaha za kemikali kuua raia wao wenyewe. Wengine wanasema kuwa tunapaswa kuzingatia zaidi juu yakupambana na magaidi wa Daesh na si kuiangusha serikali ya Syria. Marekani inalaani matumizi yoyote ya silaha za kemikali, iwe kundi la au mtu mwingine yoyote," amesema Nikki Haley.

Marekani ambayo imeshindwa kuiangusha serikali ya Syria kwa kutumia nguvu za kijeshi mara kwa mara imekuwa ikiomba serikali ya Syria iwekewe vikwazo ili kuidhoofisha na kuwapa nguvu magaidi.

Rasimu ya azimio hilo ilikuwa na nia ya kupiga marufuku biashara ya helikopta kwa serikali ya Syria, na ingewawekea vikwazo vya kiuchumi pamoja na usafiri baadhi ya maafisa wa kijeshi na wa serikali ya Syria.

Azimio hilo limeandaliwa baada ya uchunguzi wa kina uliofanywa na Shirika linalopiga marufuku matumizi ya silaha za kemikali (OPCW). Umoja wa Mataifa umethibitisha kuwa vikosi vya serikali ya Syria vilitumia helikopta kutupa mabomu ya mapipa yenye gesi ya klorin.

Nchi tisa ziliunga mkono kwa kulipigia kura azimio hilo la Braza la Usala lililowasilishwa na Uingereza, Ufaransa, na Marekani ambazo nchi hizi zinaunga mkono upande wa magaidi nchini Syria. Nchi tatu zimelipinga azimio hilo ikiwa ni pamoja na Urusi, China na Bolivia. Kazakhstan, Ethiopia na Misri hazikupiga kura kabisa. 

Serikali ya Urusi imesema kuwa magaidi ndio wamekuwa wakitumia silaha za sumu dhidi ya wananchi, na kwamba serikali ya Syria inapambana na magaidi nasi kupambana na wananchi wake.

Ili azimio la Umoja wa Mataifa lipitishwe katika baraza la Usalama, kwa kawaida linahitaji kura tisa za kuliunga mkono bila ya kupingwa na nchi zenye uwezo wa kutumia kura ya turufu ambazo ni Marekani, Ufaransa, Urusi, Uingereza na China.

Syria kwa upande wake imekana kuhusika na utumiaji wa gesi ya kemikali dhidi ya watu wake. Naibu balozi wa Syria katika Umoja wa Mataifa Mounzer Mounzer ameliambia Baraza la Usalama la umoja huo kuwa serikali ya Syria inapinga utumiaji wa silaha za maangamizi.

Mwisho wa habari/ 291

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky