Urusi na Uturuki zajadili mpango wa amani wa Syria

Urusi na Uturuki zajadili mpango wa amani wa Syria

Rais Tayyip Erdogan wa Uturuki yuko ziarani nchini Urusi kuzungumzia masuala ya Syria, huku Umoja wa Mataifa ukivilaumu vikosi vya Uturuki kwa mauaji ya zaidi ya Wakurdi 2,000 kusini mashariki mwa nchi hiyo.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Rais Tayyip Erdogan wa Uturuki yuko ziarani nchini Urusi kuzungumzia masuala ya Syria, huku Umoja wa Mataifa ukivilaumu vikosi vya Uturuki kwa mauaji ya zaidi ya Wakurdi 2,000 kusini mashariki mwa nchi hiyo.

Rais Vladimir Putin wa Urusi alimpokea mgeni wake mchana wa leo katika ikulu ya Kremlin, akisema kwamba ushirikiano wa pande hizo mbili katika kuumaliza mzozo wa Syria una mafanikio makubwa.

"Tumefurahi sana kwamba mafungamano baina ya nchi zetu mbili yanarejeshwa tena kwa haraka. Katika siku za hivi karibuni tumekuwa tukiyapandisha mahusiano haya katika kiwango ambacho kinastahiki. Tunalifanyia kazi suala la kutatuwa migogoro mikubwa sana, na wa kwanza ni wa Syria," alisema Putin.

Kwa pamoja, Uturuki na Urusi ziliwezesha kufikiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano nchini Syria mnamo mwezi Disemba, ambayo yalisaidia kupunguza kiwango cha mapigano kati ya majeshi ya Rais Bashar Assad na magaidi wanaoungwa mkono na Uturuki na Mareknai, na kisha wakawezesha kufanyika kwa duru mbili za mazungumzo kati ya upande wa rais  Assad na magaidi. Duru ya tatu ya mazungumzo inatazamiwa wiki ijayo.

Uturuki na Urusi pia ziliunganisha operesheni zao dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh au  Dola la Kiislamu nchini Syria ambalo hapo awali lilikuwa linadhaminiwa na Uturuki na Saudia arabia, na licha ya mashambulizi ya ndege za Urusi kuwauwa wanajeshi watatu wa Uturuki mwezi uliopita kwa bahati mbaya, uhusiano wa pande hizo mbili haukutetereka.

Hata hivyo, ukiacha ushirikiano wao dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh, nchi hizi zinaunga mkono pande tafauti kwenye vita hivi, ambapo Urusi na Iran zinamsaidia rais Assad kuwashinda magaidi, ambapo Uturuki, Marekani na ziko katika muungano wa nchi 61 zinazowasaidia magaidi kuiangusha serikali ya Bashar Assad. 

Uturuki yashutumiwa kwa mauaji ya Wakurdi

Mkutano huu wa Putin na Erdogan unafanyika katika siku ambayo Kamisheni ya Haki za Binaadamu ya Umoja wa Mataifa imetoa ripoti inayolikosoa jeshi la Uturuki kwa mauaji ya watu wapatao 2,000 kusini mashariki mwa nchi hiyo, ambako yanapambana na wapiganaji wa Kikurdi.

Msemaji wa mkuu wa kamisheni hiyo, Rupert Colville, anasema picha za satalaiti zinathibitisha kiwango kikubwa cha mateso na ukandamizaji uliofanywa na jeshi la Uturuki, na kwamba hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi ya waliotenda hayo.

"Picha za satalaiti za kabla na baada ya matukio hayo, ambazo zinajumuisha ripoti kutoka miji ya Nusaybin na Sur na viunga vyao, zinaonesha mitaa ikiwa imeteketezwa kabisa. Tunatiwa hofu zaidi na matokeo ya uchambuzi wa picha hizi, ambayo yanaashiria kuwepo kwa kiwango kikubwa kabisa cha uharibifu wa majengo kwa kutumia silaha nzito nzito," alisema Colville.

Mkuu wa Kamisheni hiyo, Zeid Ra'ad al Hussein, anasema kuwa katika kipindi cha kati ya Julai 2015 hadi Disemba 2016, operesheni za kijeshi za Uturuki zilihusika na uharibifu mkubwa wa makazi ya watu na uvunjaji wa haki za binaadamu, ambapo Wakurdi 500,000 wamelazimishwa kuyakimbia makaazi yao. 

Mwisho wa habari/ 291

 

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky