Urusi yalaani kitendo cha Marekani kusaidia magaidi

Urusi yalaani kitendo cha Marekani kusaidia magaidi

serikali ya Urusi imeitaka Marekani kuheshimu uhuru na mipaka ya Syria baada ya kuangusha ndege ya jeshi la Syria katika mkoa wa Raqqa. Ndege hiyo ilikuwa katika harakati za kushambulia kundi kigaidi la Daesh linalojjita dola kiislamu IS.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: serikali ya Urusi imeitaka Marekani kuheshimu uhuru na mipaka ya Syria baada ya kuangusha ndege ya jeshi la Syria katika mkoa wa Raqqa. Ndege hiyo  ilikuwa katika harakati za kushambulia kundi kigaidi la Daesh linalojjita dola kiislamu IS.

Akizungumza katika mkutano wa mawaziri wa maswala  ya kigeni mjini Beijing nchini China,waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov amesema shambulizi hilo na Marekani dhidi ya ndege ya jeshi la Syria  huenda likazidisha mzozo nchini Syria na pia kuhatarisha vita dhidi ya ugaidi. Kisa hicho  kimetokea  wakati ambapo majeshi ya Syria yameimarisha mashambulizi yake dhidi ya wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh lenye mafungamano na Marekani kusini na magharibi mwa  Raqqa, huku nalo jeshi la magaidi wa Syria lijulikanlo kama Syria Democratic forces linaloungwa mkono na Marekani likiendeleza  vita  dhidi ya serikali ya Syria ndani ya mji wa Raqqa, ambao ndio ngome ya magaidi wanaodhaminiwa na Mareknai. Katika taarifa Marekani imesema ilichukua hatua za kujilinda baada ya majeshi hayo ya Syria kuangusha mabomu karibu na  eneo linalosimamiwa na magaidi wa Syria Democratic forces ambao inawaunga mkono. Marekani pia ilijitetea kuwa haiyalengi majeshi ya Syria au Urusi, na iwapo  muungano wa vikosi vyake utahitajika kufanya mashambulizi ya kujilinda basi havitasita kuchukua hatua.

Marekani inaunga mkono magaidi

Hata hivyo kamanda wa jeshi la Syria amelitaja shambulizi hilo dhidi ya ndege ya Syria kama ushahidi wa jukumu la Marekani katika kuunga mkono wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh. Jeshi la Syria  limeonya kutokea madhara makubwa kufuatia shambulizi hilo, na kusisitiza  kuwa vitendo kama hivyo  havitalizuia kuendelea na  harakati zake za kupiga vita makundi ya kigaidi na kurejesha amani na usalama  kwa wa Syria wote. Saa chache kabla ya kuangushwa kwa ndege hiyo ya jeshi la Syria,

Marekani ilisema kuwa vikosi vinavyomuunga mkono rais wa Syria Bashar al-Assad viliwashambulia wapiganaji wa kundi la kigaidi  la Syria Democratic forces  na baadhi yao kujeruhiwa. Mapema mwezi huu, Marekani iliangusha ndege isiyo na rubani ya serikali ya Syria, baada ya ndege hiyo kushambulia magaidi karibu na kivuko cha mpaka cha al-Tanf kwenye mpaka kati ya Syria na Iraq.

Wakati hayo yanajiri jeshi la Ukombozi  la Iran limetoa onyo kali dhidi ya wapiganaji wa kundila kigaidi la Daesh wanaodhaminiwa na Marekani ,na kusema mashambulizi yeyote dhidi ya Iran yatailazimisha kutumia nguvu zaidi. Tangazo hilo lilitolewa baada ya jeshi hilo la Iran  kurusha makombora mazito yaliyolenga kundi hilo la kigaidi linaloungwa mkono na Marekani na washirika wake mashariki mwa Syria. 

Mwisho wa habari / 291

 

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky