Uturuki: hatutashirikiana na Marekani katika vikwazo vyake dhidi ya Iran

Uturuki: hatutashirikiana na Marekani katika vikwazo vyake dhidi ya Iran

Habari kutoaka Ankara zinasema kuwa, msafara wa Marekani ambao ulikwenda Uturuki kwaajili ya kufanya mazungumzo ya kushiriki katika vikwazo dhidi ya Iran, ama uturuki imetoa kauli kuwa haitashiriki na Marekani katika vikwazo hivyo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: waziri wa mambo ya nje wa Uturuki amesisitiza kuwa hawatashiriki na utawala wa Marekani katika vya upande mmoja vitakavyo wekwa na utawala wa Marekani.
Waziri huyo amesema siku ya Jumanne kwamba serikali ya Uturuki imetoa kauli kwa  viongozi wa msafara huo wakimarekani kuwa Uturuki haitashirikiana na Marekani katika vikwazo hivyo vinavyowekwa na Marekani dhidi ya Iran.
Aliendelea kubainisha kuwa: tumewaambia kuwa hatutashiriki katika hilo na tutaendelea kufanya biashara za mafuta na Iran chini ya makubaliano yetu, kwa upande mwingine amebainisha kuwa tutaendelea kukuza fungamano letu na Iran pamoja na mataifa mengine makubwa ya Ulaya kwaajili ya kuinua uchumi wa Uturuki.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky