Uturuki yaziomba Iran na Urusi kusimamisha vita Syria

Uturuki yaziomba  Iran na Urusi kusimamisha vita Syria

serikali ya Uturuki imeziomba Iran na Urusi na kuzitaka ziizuie serikali ya Syria kulishambulia jimbo la Idlib linalodhibitiwa na waasi wanaoungwa mkono na Uturuki, wakati ambapo wasiwasi unaongezeka kabla ya kufanyika mazungumzo ya amani.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: serikali ya Uturuki imeziomba Iran na Urusi na kuzitaka ziizuie serikali ya Syria kulishambulia jimbo la Idlib linalodhibitiwa na waasi wanaoungwa mkono na Uturuki, wakati ambapo wasiwasi unaongezeka kabla ya kufanyika mazungumzo ya amani.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Mevlut Cavusoglu amesema Iran na Urusi zinapaswa kutimiza wajibu wao na kuzuia mashambulizi yanayofanywa na vikosi vya serikali ya Syria katika jimbo la Idlib liliko kaskazini mwa Syria. Uturuki imekuwa ikishirikiana kwa karibu na Urusi na Iran katika juhudi za kumaliza mzozo wa Syria katika miezi kadhaa iliyopita tangu ilipojiweka mbali na Marekani na washirika wake, lakini imeongeza shinikizo kwa Urusi na Iran, kutokana na kuongezeka kwa mashambulizi katika jimbo hilo amabalo ni ngome ya mwisho ya waasi hao.

Cavusoglu amesema Uturuki imekuwa ikichukua dhamana kwa vitendo vinavyofanywa na upinzani, hivyo ni jukumu la Urusi na Iran pia kufanya hivyo hivyo kwa upande wa serikali.

''Katika siku za hivi karibuni serikali ya Syria imefanya mashambulizi Idlib na mashariki mwa Ghouta. Jana tuliwaita wawakilishi wa Iran na Urusi na kuongea nao, kwa sababu katika makubaliano tuliyoyafikia, Urusi na Iran pia wanachukua dhamana kwa utawala wa Syria, kuuzuia usiendeleze mapigano pamoja na kuzuia ukiukaji wa haki za binadaamu,'' alisema Cavusoglu.

Amesema mashambulizi hayo hauwezi ukafanyika bila ya kuwepo msaada kutoka kwa Urusi na Iran. Urusi inataka kuzileta pamoja pande zinazohusika kwenye mzozo wa Syria katika mazungumzo yatakayofanyika Sochi, mwishoni mwa mwezi huu, lakini mvutano kati yake na Uturuki, unazusha wasiwasi. Lengo kubwa la mkutano huo ni kuanzishwa kwa katiba mpya baada ya kumalizika kwa vita Syria.

Waasi waelemewa, wahitaji msaada

Katika vita vya vinavyochochewa na mataifa ya kigeni nchini Syria vilivyodumu kwa takriban miaka saba, Uturuki imekuwa ikiwaunga mkono waasi na magaidi wanaopambana na Assad, huku Urusi na Iran zikimuunga mkono Assad. Hata hivyo, licha ya tofauti hizo, Uturuki imeungana na mataifa hayo mawili yenye nguvu katika juhudi za kuleta amani ya kudumu nchini Syria, hata ingawa wachambuzi wameonya kwa muda mrefu kwamba ushirikiano huo wa pande tatu ni rahisi kuvunjika, kutokana na Uturuki kuendelea kutoa msaada kwa magaidi.

Ama kwa upande mwingine, Kamishna wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia haki za binaadamu, Zeid Ra'ad al-Hussein amesema leo kuwa vikosi vya serikali ya Syria vimewaua kiasi ya waasi 85 tangu Disemba 31, 2017 katika mashambulizi yaliyofanywa dhidi ya eneo linalodhibitiwa na waasi na ambalo limezingirwa.

Mwisho wa habari / 291


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky