Vikundi vya kigaidi vyakabidhi silaha nzito kwa majeshi ya Syria

Vikundi vya kigaidi vyakabidhi silaha nzito kwa majeshi ya Syria

Baadhi ya vikundi vya kigaidi nchini Syria yamekabidhi silaha nzito kwa majeshi ya ulinzi na usalama katika mkoa wa Diraa nchini Syria

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: vyanzo vya habari nchini Syria vimetangaza kuwa baadhi ya vikundi vya kigaidi viliokuwa na silaha vimekabidhi silaha nzito kwa majeshi ya ulinzi na usalama wa nchi hiyo katika mji wa “Jasim” uliopo ndani ya Humeh ya magharibi ya mkoa wa Diraa nchini Syria.
Aidha Chanzo hicho kwa upande mwingine kimatangaza kuwa majeshi ya usalama ya Syria yamefanikiwa kumiliki maeneo ya kijiji cha “Kharbah” na miinuko ya iliopo sehemu hiyo na ile iliopo kusini mwa mji wa Nkhal katika Humeh ya kaskazini mwa Daraa nchini humo.
Majeshi ya Syria baada ya kuukomboa na kuumiliki mkoa wa Daraa, yanafanya juhudi za kuendelea kuyakomboa maeneo mengine ya kusini mwa Syria kwa kufanya mashambulizi makali ya kijeshi na baadhi ya mida kufanya suluhu na baadhi makundi yanayojisalimisha kwa majeshi hayo nchini humo.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky