Vikwazo dhidi ya Jimbo la Wakurdi baada ya kura ya maoni ya kujitenga

Vikwazo dhidi ya Jimbo la Wakurdi baada ya kura ya maoni ya kujitenga

Safari za ndege kutoka ndani na nje ya jimbo la Kurdistan, Iraq zitasimamishwa kuanzia leo Ijumaa jioni, kwa amri iliyotoka makao makuu Baghdad, baada ya kura ya maoni iliyokuwa na utata iliyowapa wakurdi haki ya kuunda taifa lao.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Safari za ndege kutoka ndani na nje ya jimbo la Kurdistan, Iraq zitasimamishwa kuanzia leo Ijumaa jioni, kwa amri iliyotoka makao makuu Baghdad, baada ya kura ya maoni iliyokuwa na utata iliyowapa wakurdi haki ya kuunda taifa lao.

Kulingana na Mkurugenzi wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Erbil Talar Faiq Sali, safari zote za ndege za kimataifa zitasimamishwa kuanzia saa kumi na mbili jioni siku ya Ijumaa kufuatia uamuzi uliotolewa na bunge la Iraq na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Haider al-Abadi. Waziri Mkuu Haider al Abadi alitoa amri hiyo kama adhabu baada ya kura ya maoni kufanyika siku ya Jumatatu licha ya Iraq kuipinga. Takriban asilimia 92.73 walisema ndio katika kura hiyo iliyotaka uhuru wa wakurdi.

Aidha ndege nyengine kutoka kanda ya Mashariki ya kati likiwemo shirika la ndege la Uturuki, Misri na Lebanon walikwishatangaza watasimamisha safari zao kuelekea Kurdistan kufuatia ombi kutoka kwa serikali ya Iraq.

Akizungumza na waandishi wa habari, Talar Faiq Sali, Mkurugenzi wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Erbil amesema anasikitishwa na uamuzi huo, akiutaja kwamba utarejesha nyuma juhudi za kupambana na wanamgambo wa kundi la kigaidi la Daesh  nchini Iraq na katika taifa jirani la Syria pamoja na hatua ya kupeleka misaada kwa wale waliyopoteza makaazi yao kufuatia mashambulizi yanayofanywa na wanamgambo wa kundi la kigaidi la Daesh  , IS.

Amesema kuna wakimbizi wengi wanaotumia uwanja huo wa ndege na kwamba unatumiwa pia kama daraja na Syria pamoja na Umoja wa Mataifa kufikisha misaada kwa watu wanaoihitaji. Bi Faiq Sali ameongeza kuwa uwanja huo wa ndege unatumia pia na muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani kwa hiyo kuufunga au kusimamisha safari za ndege kuingia na kutoka katika uwanja huo kutamuathiri kila mtu na kwamba sio hatua nzuri iliyochukuwaliwa.

Shirika la ndege la Qatar pia limetangaza kusimamisha safari zake kuanzia tarehe 29 Septemba hadi Oktoba mosi.

Iraq inaendelea kuishinikiza Kurdistan kufuta matokeo ya kura ya maoni

Hapo jana Iraq iliiwawekea shinikizo wakurdi kuufutilia mbali matokeo ya kura ya maoni huku bunge likiihimiza serikali kuu kutuma vikosi vyake kuyadhibiti maeneo muhimu tajiri kwa mafuta, yanayoshikiliwa na vikosi vya kikurdi. Iraq kwa upande wake imeyataka mataifa jirani kukatisha operesheni zao za kidiplomasia katika mji mkuu wa Kurdistan Erbil.

Aidha kura hiyo ya maoni imeibua kitisho au hofu ya kutokea mgogoro mpya wa kikanda. Ujumbe wa kijeshi kutoka Iraq tayari unaelekea nchi jirani ya Iran kushirikiana kijeshi kama mkakati wa kulipiza kisasi unaochukuliwa na serikali ya Iraq kufuatia kura hiyo ya maoni.

Iran na Uturuki pia zinapinga hatua zozote za kujitenga kwa wakurdi na majeshi yao yameanza mafunzo ya pamoja mpakani mwa Kurdistan katika siku za hivi karibuni. Iraq na Uturuki pia wameanzisha vikosi vya kijeshi vya pamoja.

Mwisho wa habari / 291

 

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky