Viongozi mbalimbali kukutana kwenye mkutano wa usalama Ujeriuman

Viongozi mbalimbali kukutana kwenye mkutano wa usalama Ujeriuman

Viongozi wa mataifa mbalimbali duniani wanakutana katika mji wa Munich, Ujerumani wiki hii kwa ajili ya mkutano utakaozungumzia masuala ya usalama

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Viongozi wa mataifa mbalimbali duniani wanakutana katika mji wa Munich, Ujerumani wiki hii kwa ajili ya mkutano utakaozungumzia masuala ya usalama. Mgeni katika mkutano wa mwaka huu atakayeangaliwa zaidi anaweza kuwa ni waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ambaye anakabiliwa na madai mazito ya rushwa nchini mwake. Mashariki ya kati imewakilishwa vyema katika mkutano huo wa siku tatu unaoanza hii leo kwa mawaziri wa mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif na Adel al- Jubeir wa Saudi Arabia kuhudhuria mkutano huo. Hata hivyo mkutano wa mwaka huu unaweza kukosa suala muhimu la kuangazia. Waziri wa ulinzi wa Marekani James Mattis na mshauri wa masuala ya usalama Herbert Raymond McMaster wanatarajiwa kuelezea sera za masuala ya kigeni na usalama za nchini Marekani. Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Ursula von der Leyen atatoa hotuba ya ufunguzi. Hata hivyo, mazungumzo ya pembezoni mwa mkutano huo yanatarajiwa kwa mara nyingine kuwa na umuhimu zaidi kuliko hotuba. Kulingana na shirika la habari la dpa mawaziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Ufaransa na Ukraine watakutana hii leo jioni kujadili mizozo.

Mwisho wa habari / 291


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky