Viongozi wa Sudan wakubaliana kudumisha amani

Viongozi wa Sudan wakubaliana kudumisha amani

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na hasimu wake Riek Machar wamekubaliana kusitisha machafuko na kuweka amani ya kudumu. Viongozi hao wametia saini makubaliano hayo mjini Khartoum

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na hasimu wake Riek Machar wamekubaliana kusitisha machafuko na kuweka amani ya kudumu. Viongozi hao wametia saini makubaliano hayo mjini Khartoum

Viongozi mahasimu wa kisiasa nchini Sudan Kusini rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi, Riek Machar wametia saini makubaliano ya amani mjini Khartoum, ambapo chini ya makubaliano hayo, wameridhia kutekeleza katika kipindi cha saa 72 hatua ya kudumu ya kusitisha mapigano.

Hatua hiyo imeibua matumaini kwamba mkataba huo utahitimisha vita vya muda mrefu vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo. Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Al-Dierdiry Ahmed ametangaza mwafaka huo baada ya kufanyika mazungumzo katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum.

Amesema pande zote zimekubaliana usitishwaji wa kudumu wa mapigano utakaoanza ndani ya masaa 72. Kiir na Machar wamesaini waraka mbele ya rais wa Sudan, Omar Al Bashir.

Baada ya kutiliana saini, Kiir alisema hii ni siku ambayo raia wengi wa Sudan Kusini waliitarajia. Machar alisema, usitishwaji huu wa mapigano ni lazima uwe mwelekeo wa kumaliza mapigano. Juhudi mpya za amani za Sudan Kusini zilianzishwa na viongozi wa Afrika Mashariki.

Mwisho wa habari / 291

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky