Viongozi wa umoja wa mataifa washangazwa na kasi ya kuenea kwa Kipindupindu nchini Yemen

Viongozi wa umoja wa mataifa washangazwa na kasi ya kuenea kwa Kipindupindu nchini Yemen

Viongozi wa Jumuia ya umoja wa Mataifa pamoja na jumuia za misaada ya kibinadamu wanasema kuwa wameshangazwa na kuenea kwa kasi kwa ugongwa wa kipaindupindu nchini Yemen

Shirika la habari AhlulByat (a.s) ABNA: ugonjwa wa kipindupindu umezidi kuenea kwa kasi nchini Yene kutokana na uchache wa vyombo vya afya na tiba, hivyo ugonjwa huo umeshika kasi zaidi siku hadi siku nchini humo.
Kwa mujibu wa ripoti na takwimu mpya ya Jumuia ya kimataifa ya afya za binadamu ni kwamba watu zaidi ya laki 4 wamepatwa na ugonjwa huo mchini humo.
Mfumuko wa ugonjwa wa kipindupindu nchini Yemen ni tjja ya uvamizi wa kijeshi wa majeshi ya Saudi Arabia dhidi ya Yemen na kuinzigira nchini hiyo katika kila pande, kitu ambacho kimepelekea kuto patikana chakula cha kutosha, madawa na vifaa vya kitabibu.
 Kabla ya kuanza vita nchini Yemen, taifa hilo lilikuwa linahesabiwa kuwa taifa masikini zaidi miongoni mwa mataifa ya Kiarabu, ama baada ya nchi hiyo kushambuliwa kijeshi, hali hiyo imekuwa mbaya zaidi kutokana na kuharibu miundombinu ya afya nchini humo, ikiwemo ya maji safi na taka, pia jinsi ya ukusanyaji wa taka na uchafu nchini humo, mambo ambayo yamesababisha kuchafuka maji safi yanayotumika na wananchi hao na hatimaye kutokea kwa ugonjwa wa kipindupindu.
Viongozi wa Jumuia ya umoja wa Mataifa pamoja na jumuia za misaada ya kibinadamu wanasema kuwa wameshangazwa na kuenea kwa kasi kwa ugongwa wa kipaindupindu nchini Yemen.
Chama cha msalaba mwekundu kimetangaza kuwa hivi sasa kila penye wayemen 120 mmoja kati yao anashakuwa kuwa na ugonjwa wa kipindupindu.
Habari zinaeleza kuwa toka mwezi wa nne mwaka mpaka sasa, watu zaidi ya elfu 2 wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.
Mwakilishi wa shirika la afya duniani nchini Yemen amesema: vituo vya afya zaidi ya 55 nchini Yemen havifanyi kazi, kutokana na kuharibiwa vibaya na mashambulio ya wavamizi hao, ambapo baadhi ya vituo hivyo kutokana na kutokuwa na madawa na vifaa vya tiba, vimeshindwa ufanya kazi hatimaye kufungwa.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky