Vurugu dhidi ya wageni zazuka Afrika Kusini

  Vurugu dhidi ya wageni zazuka Afrika Kusini

Polisi wamefyatua leo mabomu ya kutoa machozi, risasi za mpira na mizinga ya maji wakati maandamano ya karibuni ya kuwapinga wahamiaji yalipozuka katika mji mkuu wa Afrika Kusini

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Polisi wamefyatua leo mabomu ya kutoa machozi, risasi za mpira na mizinga ya maji wakati maandamano ya karibuni ya kuwapinga wahamiaji yalipozuka katika mji mkuu wa Afrika Kusini, Pretoria. Rais Jacob Zuma amelaani vurugu hizo dhidi ya wageni na kutoa wito wa utulivu. Waandamanaji walibeba mabango wakielekea katika wizara ya mambo ya nje. Kamishena wa polisi Khomotso Phalane amesema watu 136 wamekaamtwa katika kipindi cha saa 24 zilizopita. Chuki dhidi ya wageni nchini humo wakati mwingine husababisha umwagaji damu nchini humo wakati kukiwa na tuhuma kuwa wanazichukua kazi za wenyeji. Kiwango cha ukosefu wa ajira Afrika Kusini kiko juu ya asilimia 25. Wengine wanalaumiwa kwa ulanguzi wa dawa za kulevya na uhalifu mwingine.

Mwisho wa habari/ 291

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky