Vurugu zashamili Cameroon kuelekea Uchaguzi

Vurugu zashamili Cameroon kuelekea Uchaguzi

Maafisa wa serikali ya Cameroon wametangaza amri ya kutotoka nje katika majimbo yanayozungumza Kiingereza, itakayodumu kwa saa 48. Eneo yaliko majimbo hayo linaadhimisha mwaka mmoja tangu kujitangazia uhuru.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Maafisa wa serikali ya Cameroon wametangaza amri ya kutotoka nje katika majimbo yanayozungumza Kiingereza, itakayodumu kwa saa 48. Eneo yaliko majimbo hayo linaadhimisha mwaka mmoja tangu kujitangazia uhuru.

Maadhimisho hayo ambayo hayatambuliki na serikali ya Cameroon yanakuja wiki moja kabla ya nchi hiyo kufanya uchaguzi wa rais unaotarajiwa Jumapili ijayo. Rais Paul Biya mwenye umri wa miaka 85 ambaye ameliongoza taifa hilo kwa miaka 35 iliyopita, anawania muhula wa saba madarakani.

Gavana wa eneo la Kaskazini Magharibi linalozungumza Kiingereza Adolphe Lele Lafrique amesema watu hawatarusiwa kutoka eneo moja hadi jingine kipindi cha saa 48 kuanzia Jumapili tarehe 30 Septemba hadi Oktoba Mosi.

Hatua kama hizo pia zimetangazwa katika majimbo mengine yanayozungumza Kiingereza ikiwemo mji wa Buea na Bamenda ambako viongozi wanaotaka kujitenga na kujitawala walitangaza kile walichokiita 'Jamhuri ya Ambazonia', Oktoba mwaka jana.

Hali ya kutotoka nje yatangazwa

Milipuko ya risasi imesikika Jumapili usiku katika mji wa Buea ambao ni kitovu cha uasi. Kati miji mingine ya Wacameroon wanaozungumza Kiingereza, maduka na baa ziliagizwa kufunga shughuli zao, mikusanyiko ya zaidi ya watu wanne imepigwa marufuku na usafiri umesitishwa.

Mnamo tarehe 1, 2017 tariban waandamanaji 40 wanaotaka maeneo yanayozungumza Kiingereza kujitenga na kujitawala waliuawa na Maafisa wa usalama wamewakamata mamia ya waandamanaji tangu wakati huo.

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa watu karibu 250,000 wameyakimbia makazi yao kusini magharibi na kaskazini magharibi mwa Cameroon. Kulingana na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, raia 400 wameuawa katika mzozo huo.

Mzozo bado unaendelea licha ya serikali kutuma maelfu ya askari na wanajeshi katika eneo hilo huku hamasa ya kutaka kujitawala kwa Wacameroon wanaozungumza Kiingereza ikiongezeka. Kulingana na shirika la kimataifa la kufuatilia mizozo ICG, kuna wapiganaji 1,000 wanaounga mkono azma ya kujitawala wakidhibiti maeneo makubwa ya vijijini na barabara muhimu.

Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya uchaguzi wa Oktoba saba, waasi hao wameapa hakutafanyika Uchaguzi katika maeneo ya kaskazini magharibi. Serikali imejibu kwa kusema chaguzi zitafanyika katika maeneo yote 360 ya uwakilishi.

Akizungumza mwishoni mwa juma katika kampeini mjini Maroua,Rais Paul Biya amesema nchi hiyo imefanikiwa kupambana dhidi ya waasi wanaotaka kujitenga kwa eneo linalozungumza Kiingereza pamoja na kushinda vita dhidi ya waasi wa Boko Haram, kaskazini mwa nchi.

Sulala la usalama limeibuka kuwa suala kuu katika uchaguzi ambao unatarajiwa kumpa Biya aliye madarakani tangu 1982 muhula mwingine madarakani dhidi ya wagombea wengine wanane.

Mwisho wa habari / 291

 


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky