Waarabu washirikiana na Marekani kupambana na Iran

Waarabu washirikiana na Marekani kupambana na  Iran

Viongozi kutoka nchi 40 za Kiislamu wanakutana kwa kwa mara ya kwanza mjini Riyadh, Saudi Arabia kujadili juu ya ushirikiano wa kijeshi wa nchi hizo katika juhudi za kupamabana na ushawishi wa Iran na kujadili hasara za ugaidi.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Viongozi kutoka nchi 40 za Kiislamu wanakutana kwa kwa mara ya kwanza mjini Riyadh, Saudi Arabia kujadili juu ya ushirikiano wa kijeshi wa nchi hizo katika juhudi za kupamabana na ushawishi wa Iran na kujadili hasara za  ugaidi.

Katika mkutano huo wa kwanza kufanyika, mawaziri wa ulinzi na viongozi wengine waandamizi kutoka kwenye muungano wa kijeshi wa mataifa ya Kiislamu yanayosaidia wapinzani wa Serikali ya Syria na Iraq, rasmi unahesabila kuwa ni nchi 41 ukijumlisha na Marekani ambayo ni mshirika mkubwa wa Saudi Arabia kataika kusaidia makundi yanayopambana na serikali za Syria na Iraq. Kwa ushirikiano kundi hilo lina msimamo wa pamoja dhidi ya iran na washirika wake . Umoja huo wa kusaidia waasi ulianzishwa mnamo mwaka 2015 chini ya uongozi wa mwana mfalme Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia, ambaye hadi sasa amepanda kwa kasi mno tangu kuteuliwa kwake kuwa mrithi wa kiti cha enzi mnamo mwezi Juni hali ambayo imetikisa jukwaa la kisiasa katika kanda yote ya Mashariki ya Kati.

Mohamed bin Salman ambaye pia ndiye waziri wa ulinzi wa Saudi Arabia katika hotuba yake ya ufunguzi ameapa kuwafuatilia magaidi mpaka watakapomalizika kabisa duniani. Katika mkutano huo Luteni jenerali Abdallah al Saleh wa jeshi la Saudi Arabia ameteuliwa kuwa katibu mkuu wa Umoja huo wa kijeshi wa nchi za Kiarabu dhidi ya kile wanachodai kuwa ni Ugaidi( IMCTC) naye kwa upande wake amesema ushirikiano huo wa kijeshi utakuwa wazi kwa nchi nyingine ambazo zitataka kujiunga nao.

Saleh amesema mataifa yanayounga mkono yatakuwa na fursa, kuwa na makubaliano rasmi ya pande mbili, nchi hizo zitaweza kuwa na wawakilishi wao ndani ya muungano pia watakuwa na haki ya kutoa mipango yao wenyewe na vilevile kutathmini baadhi ya mipango inayojadiliwa na wanaweza kuchangia mipango hiyo kifedha au kitaalam.

Mkutano huo ulioanza jana Jumapili unafanyika wakati ambapo ushirikiano wa kijeshi pamoja na mshirika mkuu wa Saudi Arabia ambaye ni Marekani, wamo katika vita dhidi ya Serikali za Syria, Iraq na Yemen.  Ambapo umoja huo unatumia makundi  ya kigaidi kujaribu kuziondoa serikali za Syria na Iraq madarakani, kwa lengo la kuidhoofisha Iran na ushawishi wake katika nchi za kiarabu.

Mkutano huo ambao kwa kiasi kikubwa hauzingatii nchi zinazofuata madhehebu ya Sunni pekee hata hivyo umeitenga Iran nchi inayofuata madhehebu ya Shia ambayo ni hasimu na mpinzani wa Saudi Arabia. 

Syria na Iraq pia zimetengwa kutokana na viongozi wake kuwa na uhusiano wa karibu na Iran. Hali hiyo inadhihirisha juu ya kuongezeka kwa mvutano kati ya Saudi Arabia na Iran, hususan juu ya vita katika nchi za Syria na Yemen pamoja na hali ya kisiasa ya nchini Lebanon.

Saudia Arabia na washirika wake kutoka nchi zaidi ya 40 wanasaidia magaidi nchini Syria na Iraq ambapo Iran inazisaidia serikali kupambana na magaidi hao.

Na huko yemen saudia Arabia na washirika wake wanafanya mashambulizi dhidi ya wananchi wa Yemen na kumuunga mkono rais Haadi ambapo Iran inaunga mkono wananchi wa Yemen.

Nchi za kiarabu , Marekani na washirika wao wamepata hofu kubwa baada ya majeshi ya Iran na washirika wake kuyasambaratisha na kuharibu utawala wa makundi ya kigiaidi  yanayodhaminiwa na umoja huo, nchini Syria na Iraq.

Mwisho wa habari / 291

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Arba'een
Mourining of Imam Hossein
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky